Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Triple H mfalme wa mieleka

Muktasari:

Katika kudhihirishia mashabiki wake kuwa yeye bado ni tishio katika ulingo katika mechi yake ya hivi karibuni alimshinda mkongwe mwenzie Goldberg na kutwaa mkanda wa ubingwa wa uzito wa juu.

CONNECTICUT, Marekani

KATIKA nyota kumi bora waliowahi kutokea katika mchezo wa mieleka, hauwezi kulikosa jina la Paul Michael Levesque ‘Tripple H’, mfalme wa  wafalme wa mieleka.

Uwezo wake unaendana kabisa na sifa alizo nazo. Kwani hadi kufikia sasa, mwamba huyu tayari amejizolea mataji 23. Miongoni mwa mataji hayo ni pamoja na yale ya ubingwa wa shirikisho la dunia la mieleka mara nane, ubingwa katika uzito wa juu mara tano, ubingwa wa mabara mara tano, ubingwa wa Ulaya mara mbili. Pia amewahi kushinda katika mechi walizocheza kama timu mara tatu katika mashindano tofauti tofauti.

Licha ya ukorofi alionao, lakini ni mtu anayeheshimika sana katika fani hiyo ya mieleka. Kwa sasa ni miongoni mwa viongozi wa juu wa shirikisho la mieleka duniani akifanya kazi kama makamu wa rais wa vipaji na maonyesho ya wazi.

Katika nafasi hiyo ameibua na kuendeleza vipaji kadhaa vya mchezo huo na hilo hasa lilikuwa lengo lake anasema.

“Ningependa kuona kina Tripple H wengine wanazaliwa kwa kipindi cha miaka ijayo na kuuendeleza mchezo huu. Hivyo ni jukumu letu kwa sasa kuhakikisha hili linafanyika kwa ufanisi,” anasema Tripple H.

Tripple H ni baba wa watoto watatu na pia ni mume halali wa Stephanie McMahon ambaye ni mtoto wa Vincent Kennedy “Vince” McMahon promota maarufu wa mchezo huo, Mkurugenzi Mtendaji na pia mwenyekiti ya bodi ya kamati ya Stamford, Connecticut, inayojishughulisha na kukuza mchezo wa mieleka duniani.

Mashabiki wake wanamwelezea Triple H kama mtu asiyewezekana katika suala zima la mieleka. Ni mbaya sana awapo ulingoni.

Mwanzo wa  Triple H
Mtu anayejulikana kama Triple H alizaliwa akiwa Paul Levesque mnamo Julai 27, 1969 huko Greenwich, Connecticut nchini Marekani. Akiwa na umri wa miaka 14, alikuwa akipenda sana mchezo wa kutunisha misuli, jambo ambalo lilichangia kumfanya aingie kwenye mchezo huo akiwa mdogo sana.

Mwaka 1988 akiwa na umri wa miaka 20 tu alifanikiwa kutwaa taji la Mr. New Hampshire na hapo ndipo safari yake ya kuwa mwanamieleka ilipoanzia.

Kufikia heshima aliyokuwa nayo leo hii haikuwa kazi rahisi hata kidogo. Baada ya kujiweka sawa katika kutunisha misuli, aliona ipo haja ya kwenda kujifunza kuhusiana na mieleka. Na hapo ndipo alipoamua kwenda shule kupata ujuzi zaidi.

Paul alipitia shule ya mieleka ya Killer Kowalski na baada ya kuhitimu, mwaka 1992 alijiunga na shirikisho la mieleka la kujitegemea (IWF).

Kwa kuwa kila mpiganaji alikuwa na jina lake la ulingoni wakati huo alikuwa ulingoni alijulikana kama Terra Ryzing. Baada ya kuwa bingwa wa IWF, aliona ipo haja ya kushiriki katika Word Championship Wrestling (WCW).

Akishiriki katika WCW, Paul Levesque alibadilisha jina lake na kujiita Jean-Paul Levesque na kutumia jina la Sbobby kama jina lake la ulingoni.

Akitumia jina hilo alipigana kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya kujiita Tripple H ikiwa ni kifupi cha maneno ( Hunter Hearst Helmsley). Pamoja na vibweka vyake kadhaa katika mchezo huo kama vile kupenda wasichana, mtu wa fujo bado haikumwondolea sifa ya kuwa miongoni mwa wanamieleka wanaopendwa siyo tu nchini Marekani bali duniani kwa jumla.

Mafanikio ya Triple H
Mashabiki wa mchezo wa mieleka duniani wanamtambua kama mkali wa kupigana kwani amekuwa mbishi aingiapo ulingoni. Siyo rahisi kumshinda, unahitajika kuwa na utaalamu wa ziada kama unataka kumshinda mwamba huyu.

Licha kupigana akiwa peke yake na kufanikiwa kushinda mataji kibao,  aliungana na wakali wengine kama Steve Austin na kuchukua ubingwa wa  World Tag Team.
Hivi karibuni mwamba huyo ameungana na wanamieleka wakongwe, Ric Flair, Randy Orton na Batista na kuunda timu yao inayoitwa ‘Evolution’.

Katika kudhihirishia mashabiki wake kuwa yeye bado ni tishio katika ulingo katika mechi yake ya hivi karibuni alimshinda mkongwe mwenzie Goldberg na kutwaa mkanda wa ubingwa wa uzito wa juu.

Usilolijua kuhusu Triple H
Kabla ya kuingia kwenye ulimwengu wa mieleka, alikuwa mchoraji kazi,  ambayo aliitelekeza.
Ule muziki unaopigwa kama kiashirio cha yeye kuingia kwenye pambano unaofahamika kama The Game, umepigwa na bendi moja ya muziki wa Rock ya nchini Uingereza inayofahamika  ‘The Metal Band, Motorhead’.

Gari analolipenda zaidi kuliko yote ni Hummer yenye rangi nyekundu.
Licha kuwa mwanamieleka, Triple H pia ni muigizaji wa filamu. Miongoni mwa filamu alizoigiza ni pamoja na Inside out, Pacific na Blade: Trinity.