Aishi maisha magumu na wanaye, vitu vyote vyauzwa

Liliani Daniel Nyihocha (36) akinyonyesha kwa zamu watoto pacha kutokana na kutokuwa na maziwa ya kutosha kwa kuwa hana lishe nzuri
Muktasari:
Akiwa na watoto pacha aliokuwa amejifungua mwezi mmoja na wengine watatu, alinyang’anywa kila kitu kuanzia vifaa vya malazi, kupikia, kulimia, mifugo, madaftari, sare za watoto na kusababisha kutokwenda shule, vyote vikauzwa na si kwamba alikuwa na deni katika taasisi ya fedha.
Serengeti. Maisha ya familia ya Lilian Daniel Nyihocha (36) mkazi wa kitongoji cha Kazi, Kijiji cha Rwamchanga Kata ya Manchira Wilaya ya Serengeti, Mkoa wa Mara, yalibadilika kutoka familia ya watu wenye uwezo kuwa ombaomba.
Akiwa na watoto pacha aliokuwa amejifungua mwezi mmoja na wengine watatu, alinyang’anywa kila kitu kuanzia vifaa vya malazi, kupikia, kulimia, mifugo, madaftari, sare za watoto na kusababisha kutokwenda shule, vyote vikauzwa na si kwamba alikuwa na deni katika taasisi ya fedha.
Ilikuwa ni adhabu iliyotolewa kwa mume wake, ambaye alikamatwa kwa tuhuma za kumvamia mwalimu wa Shule ya Msingi Rwamchanga kwa lengo la kuiba fedha za kikundi cha Benki ya Hifadhi ya Jamii ‘Community Conservation Bank (COCOBA)’.
Adhabu ambayo inakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 12-6) (e) ambayo inabainisha kuwa ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama ama kupewa adhabu zinazomtesa au kumdhalilisha.
Ilivyokuwa
Akiwa anahangaishwa na watoto wake pacha wenye umri wa miezi sita na mwingine wa miaka mitatu wakihitaji kula, huku akijitahidi kuwabembeleza kwa kuwapa viazi vibichi walivyopewa na bibi yao, wanapoanza kuhangaika kutafuna, anapata nafasi ya kuanza kusimulia matatizo yalivyowakuta.
“Machi 31 mwaka huu alfajiri kundi kubwa la wananchi lilifika hapa likidai mume wangu Umbuya Obonyo (42) anatuhumiwa kumvamia mwalimu wa shule ya msingi ambaye ni mtunza hazina wa Cocoba….na kuingia ndani yanyuma na kutoa kila kitu wakaenda kuuza,” anasema.
Huku akilengwa machozi anapoonza kueleza, huku watoto wakililia chakula, mahojiano yanasimama kwa muda, kisha anasema hakuwa na muda wa kupata ufafanuzi wa adhabu hiyo inayohusu familia wala si mtuhumiwa, iweje waadhibiwe wao.
“Mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji Joseph Makuru, sikusikilizwa hata nilipowaambia waniachie hata kitanda kimoja…hawa pacha walikuwa na mwezi mmoja wamezaliwa, walitolewa kitandani na kuwekwa kwenye sakafu…wakachukua vitanda, magodoro na kila kitu kilichoonekana mbele yao…ikiwemo nguo zetu za ndani,” anasema na kuongeza:
“Vyombo vya kupikia, majembe, mabati matano, mapazia, ng’ombe wawili, mbuzi watatu, kondoo watano, mazao ya chakula, kuku 32 akabaki mmoja…sare za wanafunzi ikiwemo madaftari, viatu…walituacha na nguo tulizokuwa tumevaa...ndanihawakuacha hata kijiko, baadhi wakaanza hata kubomoa nyumba….nilishindwa niwafanyeje hawa watoto, wale, walale wapi na tutapikia nini,” anasema kwa uchungu.
Lilian anasema mume wake alipelekwa kituo kidogo cha polisi Rwamchangakisha akapelekwa Mugumu na kufikishwa mahakamani, na hakupata dhamana mpaka sasa anaendelea na kesi yake, lakini yeye anajiona ana mateso makubwa kuliko hata aliyeko mahasubu kwa mzigo alionao akiwa hana kitu.
“Vitu vyangu vilichukuliwa na watu na vingine kuuzwa siku hiyo hiyo chini ya uangalizi wa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji na mwenyekiti wa yote Joel Makori. Walifanyia uwanja wa Shule ya Msingi Rwamchanga, licha ya watu kuwasihi kuwa ni mwiko kwa mila na desturi kumnyang’anya mtu mpaka mwiko na kuuza hawakusikiliza, wakauza,” anabainisha.
Akiongea kwa hisia anasema pamoja na kuwa alikuwa hajapona mkono uliovunjika akiwa mjamzito na alikuwa hajaanza kufanya kazi ngumu, analazimika kufanya kazi mbalimbali ili kunusuru maisha ya watoto wake watano, kwa msaada wa majirani waliompa vyombo vya kupikia, chakula huku wakilala chini, hawana mavazi, watoto wawili wa darasa la sita na kwanza wakasitisha masomo.
Anusuriwa na mama yake
Hali zao zilizidi kuwa mbaya ikalazimu mama yake mzazi kuwachukua na kuhamia kwao walikokaa kwa miezi miwili ili apate nguvu, huku ndugu na jamaa waliokuwa wakienda kumsalimia wanamchangia mithili ya mfiwa, akapata fedha za kuwanunulia watoto wake sare na madaftari, wakaanza masomo.
“Mwanangu mkubwa Hapinnes (12) anayesoma darasa la sita ndiye ananisaidia majukumu…Fredy (8) alikuwa darasa la pili nikaomba walimu arudi la kwanza ili awe anapata muda wa kunisaidia kazi ...maana ili nitoke kutafuta mahitaji madogo mpaka atoke shule abaki na wadogo zake,” anasema Lilian.
Juhudi zake za kufuatilia mali zake zilizouzwa kwa uongozi wa kijiji zilikutana na vitisho vya kutengwa kwa kuwa mkakati wake unaweza kukiweka kijijikatika mazingira magumu na kulazimika kumlipa.
Christina Nyihocha (62) mama mzazi wa Lilian kwa masikitiko anasema uamuzi wa kukamata vitu vya ndani ni tukio la kwanza kutokea:
“Hofu ya kutengwa na jamii ndiyo imetanda, maana mtuhumiwa alikamatwa na yuko mahabusu ...inakuwaje mke na watoto hawa wachanga nao waadhibiwe…maisha anayoishi mwanangu huyu ni ya mateso makubwa…na sisi ndiyo tunawahudumia,” anasema kwa masikitiko.
Wakati suala hilo likiwa ni gumzo kijijini hapo licha ya kuwepo vitisho, baadhi ya viongozi wamekuwa wazi kusema kuwa uamuzi wa kukamata mali za Lilian kisha kuuza ni ukiukwaji wa haki za Binadamu na uvunjwaji wa misingi ya utawala wa sheria.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Joseph Makuru anakana kuwahawakukamata mali yoyote ya mtuhumiwa na kuuza ingawa alikuwa anaongoza wananchi kufuatilia na kufika kwa Lilian.
Katika mahojiano ofisini kwake Mwenyekiri huyo akitoa kauli zinazokinzana anadai kuwa hawakukamata mali hizo, lakini anapobanwa kuwa wananchi wanakiri kuchukua vitu na kuuza na kisha fedha kumpa mwalimu aliyedaiwa kuvamiwa kwa ajili ya matibabu.
“Inawezekana waliuza mimi nilipotoka…maana kuchukua mpaka vitu vya ndani ni laana”, anasema.
Aliyesimamia uuzwaji akiri
Joel Makuri aliyesimamia uuzwaji amemthibitishia mwandishi wa habarikuwa vitu vyote viliuzwa kwenye uwanja wa shule na Mwenyekiti waSerikali ya kijiji alihusika na walipata sh 500,000 akakabidhiwa mwalimu aliyevamiwa kwa ajili ya matibabu na kuwa ilikuwa ni hasira za wananchi.
“Tuliuza hata polisi wanajua …maana nikiwa na mwenyekiti wa Serikali ya kijiji, mwenyekiti wa Ritongo tuliitwa polisi na kukiri kuuza…wakasema tuondoke yeye aendelee na kesi yake…baadhi ya vitu tulimrudishia Lilian kama vitanda viwili, sufuria tatu, pipa moja na godoro ili atumie”, anasema.
Hata hivyo taarifa yake inapingwa na Lilian, mama yake na majiranikuwa hawakumrudishia hivyo vitu anavyosema na kuwa hiyo ni njia yakujikosha,kwa kuwa alilala chini na wanae kwa muda mrefu mpakaakachukuliwa na ndugu zake.
Mwenyekiti wa Ritongo Joseph Daniel anakana kuhusika kwa kuwa hakuwepona hata walipokwenda polisi hakuwa nao.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kazi Jumanne Mahiti anadai wakati tukio linatokea hakuwepo alikuwa nchini Uganda, lakini anakiri mali za Lilian kukamatwa na kisha kuuzwa katika eneo la shule.
Mwenyekiti wa shirika la Wasaidizi wa Haki za Binadamu Serengeti Samweli Mewama anakiri kupokea malalamiko ya Lilian na kuwa wanaendelea na ufuatiliaji.
“Ibara ya 24-(1)na (2) bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1)nimarufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake madhumni yakuitafisha au madhumni mengineyo bila idhini ya sheria ambayo inawekamasharti ya kutoa fidia inayostahili”anasema.
Anasema haki ya kumiliki mali imefafanuliwa katika sheria ya 1984Na.15 ibara 6 ,sheria ya 2005 Na.1 ibara 9,hivyo waliohusika wanapaswakushitakiwa kwa kuwa vyombo vya kijamii vimekuwa na madhara makubwakwa jamii kwa kutumia nguvu badala ya sheria ,kwa kuwa suala lamtuhumiwa linapaswa kuendelea mahakamani lakini kuuza mali ni kosakubwa.
Kwa watakaoguswa kumsaidia wawasiliane kwa simuyake namba 0769583988,0687684856 au mwandishi wa habari 0787239480.
Itaendelea.