Mbowe, Mnyika na Heche watia timu Tarime

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, John Mnyika na wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya chama hicho wamewasili mjini Tarime tayari kuhutubia mkutano wa hadhara unaofanyika Uwanja wa Sabasaba maarufu kama Shamba la Bibi mjini Tarime.

Tarime. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, John Mnyika na wajumbe kadhaa wa Kamati Kuu ya chama hicho wamewasili mjini Tarime tayari kuhutubia mkutano wa hadhara unaofanyika Uwanja wa Sabasaba maarufu kama Shamba la Bibi mjini Tarime.

Pamoja na Mbowe, wengine waliowasili ni Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), John Pambalu, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Sharifa Suleiman, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee (Bazecha), Hashimu Issa Juma na mjumbe wa Kamati Kuu, John Heche ambaye ni mwenyeji wao.

Katika msafari huo, pia wamo mbunge wa zamani wa chama hicho kikuu cha upinzani akiwemo Joyce Mukya na Meya wa zamani wa Ubungo, Boniphace Jacob.

Mkutano wa leo Jumatatu Januari 23 ni wa tatu tangu chama hicho kilipozindua mikutano yake jijini Mwanza Jumamosi Januari 21.
Mkutano wa pili wa hadhara wa Chadema ulifanyika mjini Musoma jana Jumapili Januari 22, 2023.