Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UVCCM yawataka vijana kuepuka kutumika vibaya na wasaka uongozi

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Yuvenal Shirima akizungumza na vijana Kata ya Kilema Kati.

Moshi. Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, umewataka vijana kujiandaa kugombea nafasi za ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu ujao, huku wakisisitiza umuhimu wa kuepuka kutumika vibaya na watu wanaotafuta masilahi binafsi kwa kuwatumia kisiasa.

Wito huo umetolewa leo, Aprili 6, 2025, na Mwenyekiti wa UVCCM Moshi Vijijini, Yuvenal Shirima, alipokua akizindua mashindano ya Yuvecup League katika kata ya Kilema Kati, wilayani humo.

"Tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu, niwaombe vijana wenzangu utakapofika wakati tukajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za udiwani na ubunge.

“Ni haki ya kila mwanachama kuchagua na kuchaguliwa. Tunataka vijana mjitokeze kwa wingi, na mimi kama mwenyekiti wenu, nitaendelea kuwasemea," amesema Shirima.

Pia, Shirima amesisitiza kwamba ni muhimu kwa vijana kuhakikisha wanachagua na kuchaguliwa viongozi wanaoishi katika maeneo yao na wanaojua changamoto zinazowakabili wananchi.

"Vijana tuepuke kutumiwa vibaya kisiasa, tuwe waangalifu tusirubuniwe kwa fedha na kuwachagua watu ambao hawajui kero za maeneo yetu. Tusiwachague watalii, watu wanaotoka mikoa mingine, na wanapofika kipindi cha uchaguzi ndipo wanajitokeza kutaka kugombea.

Ameongeza kuwa viongozi wanaotoka katika maeneo husika wanaweza kutekeleza ahadi zao kwa ufanisi zaidi, kwani wanazifahamu changamoto za wananchi kwa kuziishi na kukutana nazo kila siku.

Katika hatua nyingine, Shirima amewakumbusha vijana kujivunia kazi zinazofanywa na Serikali katika maeneo yao ili wananchi waweze kuzifahamu na kuendelea kuiamini Serikali.

Kwa upande wake, Sophia Shoo, mmoja wa vijana waliohudhuria mkutano huo, amesema kuwa vijana ni kundi muhimu katika jamii na ikiwa watajipanga vizuri kuelekea uchaguzi, wanaweza kuleta mabadiliko chanya.

"Tunatakiwa kujitambua kuwa sisi ni kundi muhimu, na katika kuelekea uchaguzi tunapaswa kujipanga vizuri ili kupata viongozi bora watakaotuvusha mbele," amesema Shoo.

Naye, Godlisten Thomas, mmoja wa washiriki wa mashindano ya Yuvecup, ameelezea jinsi michezo inavyowasaidia vijana kukaa pamoja, kubadilishana mawazo na kuepuka makundi maovu ya mitaani.