Majibu mwanana kwa wasomaji

Tuesday February 25 2020

Faustin Malibo anapiga simu kwa Mhariri wa Jamii. Anasema: “Ninyi mnasema ni independent (huru). Wapi? Mnaandika kwa woga. Kama ni huru mbona hamwandiki makubwa tunayoona yanatendeka?” Anasonya na kukata simu.

Siku mbili baadaye mtu mmoja ali-yesema anaitwa Ebenezer (jina moja) akaita na kusema “…mnaandika kwa kushangilia pale wadogo wanapoka-bwa koo; lakini ya wakubwa hamyaoni.

Mungu anawaona.”Lakini aliyejitambulisha kuwa ni Paulina Ruhubya wa Gongoni, Tabora mjini anasema, “hili gazeti lilijitambu-lisha kuwa na wananchi na jina lake linaonekana hivyo.“Mbona hatuoni mkiandika kutoka vijijini mkiongea na wakulima; kujua matatizo yao na kuyaandika gazetini ili watawala wayaone na kuchukua hatua?” anauliza Paulina na kuonge-za, “habari ni zile za Dodoma, Dar es Salaam, makao makuu ya mikoa na wilaya. Tatizo ni nini?” Haya ni maswali matatu miongoni mwa 11 yaliyoulizwa wiki iliyopita ambayo inamalizikia tarehe 17 Feb-ruari.

Nimechukua haya kwanza kwa sababu yanalenga kitu muhimu: haki ya watu kupata taarifa. Mengine tuta-yajibu hatua kwa hatua.Nikiri kwamba hakuna kitu kigumu kama kujaribu kujibu swali ambalo hukulielewa au ambalo halipo. Utaba-ki palepale, akili ikikuzunguka kama wacheza ukiti.

Hii ni kwa kuwa hukupata pia mwan-ya wa kuhojiana na anayeleta swali ili uelewe urefu na upana wa anachosema na kupata hata mifano.Malibo ambaye hata kwa sauti alisikika mkali, anasema tunajigamba kuwa gazeti huru lakini haoni uhuru huo. Anasema hatuandiki makubwa anayoona yanatendeka.

Meza ya Mhariri wa Jamii inamwom-ba Malibo atufafanulie mambo mawili: Kwanza, anaelewa nini kwa gazeti kuwa huru. Pili, Meza inamwomba asaidie kuo-rodhesha yapi “makubwa” ambayo gazeti halioni; makubwa kiasi gani, makubwa kuliko yapi; na makubwa kwa wema na uzuri; au makubwa kwa ubaya. Huyu hachomoki. Kwa ufafanuzi atakaoutoa, Meza itawasilisha hapa majibu sahihi yatokananyo na ufaha-mu mpana.Ebenezer anadai gazeti “linashan-gilia pale wadogo wanapokabwa koo; lakini ya wakubwa hamyaoni. Mungu anawaona.”

Advertisement

Ili kupata majibu,swali liwe kamilina ikiwezekanaliwe na mifano yaunachotaka auunacholalamikia.Hakika Mungu anatuona. Mlalamik-aji hasemi wadogo ni wapi, wamefanya

 nini na wamefanyiwa nini.Hasemi wakubwa ni wapi, wamefan-ya nini na wamefanyiwa nini; au gazeti limefanya nini. Je, gazeti limeshangilia nini na vipi?Bila shaka kukabwa koo ni kuminywa; ni kuzibwa hewa na kunuia kuanga-miza. Nani ametendewa hivyo, yuko wapi, taarifa zake ziko wapi; nani anajua hayo yametendeka; nani anajua kuwa gazeti limejua hayo na limekaa kimya?Bila majibu kwa maswali hayo, hoja au madai ya Ebenezer yanabaki bila nuru ya ukweli na usahihi. Ni mpa-ka hapo atakapofunguka na kuwa na shabaha ya kuwasilisha anachokijua fika, ndipo Meza ya Mhariri itaweza kutoa jibu.Paulina Ruhubya anataka kuona habari za vijijini katika Mwananchi na “juhudi ya mwandishi kwenda hadi pembezoni mwa nchi” na kukaa na wakulima, kujua hali zao, kuandika taarifa juu yao na kuzichapisha. Ukweli ni kwamba habari za vijijini zinapatikana katika gazeti hili, lakini siyo nyingi.

Waandishi walio karibu na vijiji wamekuwa wakiandika habari za wananchi – matatizo, furaha yao na mafanikio.Aidha, kutokana na mfumo wa mawasiliano wa sasa, taarifa nyingi za wananchi zinafika moja kwa moja chumba cha habari kutoka kwa wanan-chi, viongozi ngazi za chini au waandi-shi wetu. Kinachohitajika pale ni kuta-futa ushahidi na uthibitisho wa kina-chodaiwa kuwepo.

Huko tuendako, ambapo wanan-chi wengi popote walipo watakuwa wanapokea na kupeleka taarifa kwa chombo kidogo mikononi mwao (simu), tofauti kati ya walio shamba na walio majijini, kwa upatikanaji wa taarifa, itakuwa ndogo au itaondoka kabisa.Bali Paulina amenikumbusha enzi zile nikiwa ripota.

Nikitoka chumba cha habari jijini Dar es Salaam na kwenda kuishi na kufanya kazi na wakulima; nikiandika juu yao na kazi zao; waki-jisoma kwenye magazeti nikiwa bado ninao hapo vijijini na baadhi ya kero zao kutatuliwa nikiwa pamoja nao.

Kama sasa unaweza kuwafikia kwa sekunde; kuongea nao kama aliyenao sebule moja, umuhimu wa kuwa pamo-ja utaletwa na kitu kikubwa zaidi ya kutafuta taarifa – kama kujifunza jinsi wanavyoishi.

Mhariri wa Jamii anapatikana: 0763670229

Advertisement