Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashindano ya shule yarudishwe

Muktasari:

Kama hiyo haitoshi, kuwe na vipindi vya michezo katika ratiba ya siku ya masomo kama ilivyokuwa miaka hiyo (maarufu kama vipindi vya PE) ili msisitizo uanzie hapo. Hilo litawafahamisha wachezaji kwamba michezo ina umuhimu kama masomo mengine na kwamba pia ni ajira.

Serikali ya awamu ya nne iliyarudisha mashindano katika ngazi za kitaifa kwa shule za msingi na sekondari ambayo katika miaka ya 70 hadi 90 yalizalisha wachezaji wengi mahiri ambao walichangia katika kuzifanya timu zetu za mpira wa miguu katika ngazi ya klabu au taifa kuwa tishio katika soka la Afrika.

Ni ukweli usiopingika kwamba pamoja na michezo hiyo kurudishwa kwa takribani miaka 12 sasa, msisimko wake ni mdogo na hili linatokana na mambo yafuatayo:

Shule kutokuwa na walimu wa michezo weledi: Kila shule iwe na mwalimu wa michezo aliyesomea kazi hiyo.

Hii kwa sasa inawezekana ikizingatiwa kwamba Chuo cha Michezo cha Malya, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na walimu wengi wa shule za msingi na sekondari ambao wamehudhuria mafunzo ya ukocha katika ngazi za awali, kati na pevu wapo wengi kwa sasa.

Kama hiyo haitoshi, kuwe na vipindi vya michezo katika ratiba ya siku ya masomo kama ilivyokuwa miaka hiyo (maarufu kama vipindi vya PE) ili msisitizo uanzie hapo. Hilo litawafahamisha wachezaji kwamba michezo ina umuhimu kama masomo mengine na kwamba pia ni ajira.

Kutokuwapo kwa maandalizi ya muda mrefu ya timu: Mara nyingi maandalizi ya michezo hii kuanzia katika ngazi ya shule, kata, wilaya mkoa na kanda yanaandaliwa kwa muda mfupi.

Sababu kubwa ya kufikia hali hiyo ni kukosekana kwa mipamgo mizuri na hivyo kutopata timu zenye nyota.

Kutokana na ukweli huo, nashauri yafuatayo yafanyike au yapewe angalizo zaidi:

Kuwe na maandalizi ya muda mrefu ya mashindano ambayo yatasaidia kuibua vipaji vyote ambavyo vipo kwenye mchezo wa mpira wa miguu.

Hili likipangwa vizuri, linaweza lisisababishe gharama na kutowapotezea wanafunzi muda wa kusoma.

Kwa bahati nzuri, shule siku hizi ziko jirani hivyo kama mpango umepangwa vizuri, mathalan shule mbili zishindane michezo minne, walimu watakuwa na nafasi ya kuwaangalia wachezaji kwenye mechi nne hivyo wachezai wanaostahili kupatikana.

Baada ya hapo, shule katika ngazi ya kata zitakuwa zimewatambua wachezaji wao mahiri wa soka, bila ya kujali wanacheza nafasi moja, kwani wakati wanaunda timu ya kata watachujwa.

Michezo kama hii inaweza kuchezwa siku za mwisho mwa juma tu.

Wakati fainali zinafanyika katika ngazi ya kanda, wawepo walimu ambao wana vyeti vya ngazi pevu ya ukocha au leseni ya CAF ili kuwateua wachezaji ambao wana uwezo wa kutosha hivyo kuwa na fainali za kitaifa ambazo zitakuwa zimejumuisha wachezaji wote mahiri.

Wakati wa mashindano ngazi ya Taifa, kuwe na jopo la makocha waandamizi ndani ya umoja wa shule za msingi au sekondari na wale kutoka TFF (hususan makocha wa timu za Taifa za vijana), ambao watafanya kazi mbili.

Kuwachagua wachezaji wa timu za Taifa za Umitashumta na Umiseta na wengine kuchaguliwa timu za Taifa za vijana (U-17 na U-20) moja kwa moja.

Maana yake hapa ni kwamba, michezo ya umoja wa shule za mMsingi na sekondari baina ya mataifa (zamani yalikuwepo ya sekondari) irudishwe.

Wakati ule wachezji walijituma ili kuchaguliwa kwenye timu ya taifa ya wanafunzi ambayo ilishindana na timu za mataifa mengine.

Kwa kuanzia, ndani ya Cecafa michezo hii inaweza kuandaliwa kupitia dawati la Jumuia ya Afrika Mashariki ili yapewe kipaumbele kisekta.

Uzoefu katika kufundisha soka unaonyesha kwamba uelewa wa haraka na ubunifu wa mchezaji uwanjani unachangiwa kwa kiwango kikubwa na elimu ya mchezaji husika. Ni wachezaji wachache wenye vipaji vya hali ya juu ambao wanaweza wakawa na utimamu huo niliosema. Tukiboresha michezo hii tutapata nafuu mapema na kuunda timu bora na shindani za Taifa za mpira wa miguu.