Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matumizi ya umeme jua ndio mpango mzima kwa sasa

Katika miaka ya karibuni, nishati ya umeme jua imekuwa mkombozi kwa wakulima wengi nchini Tanzania.

Kupitia maendeleo ya teknolojia, wakulima wanaweza kufaidika na njia mbadala za umeme ambazo zinasaidia kupunguza gharama za uzalishaji na kuimarisha kilimo endelevu.

Matumizi ya umeme jua katika sekta ya kilimo yanaongezeka kwa kasi, huku wakulima wakichukua hatua za kuwekeza katika teknolojia zenye manufaa ya muda mrefu.

Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) zinaonyesha, Tanzania ni moja ya nchi za Afrika Mashariki zilizo na mwamko mkubwa katika matumizi ya umeme jua kwa shughuli za kilimo.

Kwa mujibu wa ripoti ya FAO ya mwaka 2022, zaidi ya asilimia 25 ya wakulima wadogo walitumia umeme jua kwa shughuli mbalimbali, ikiwemo umwagiliaji wa mazao.

Hii inawasaidia kuepuka gharama za umeme wa kawaida au jenereta zinazotumia mafuta, ambazo mara nyingi ni ghali na hazipatikani kirahisi vijijini.

Kama inavyoelezwa katika ripoti ya Mamlaka ya Nishati na Maji Tanzania (Ewura) ya mwaka 2023, umeme jua una faida nyingi kwa wakulima.

Mosi, unapunguza gharama za uzalishaji kwa kuwa nishati ya jua ni bure na inapatikana kwa wingi.

Kwa mfano, matumizi ya pampu za maji zinazoendeshwa na umeme jua yamepunguza gharama za umwagiliaji kwa asilimia 40 katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Hii imeleta unafuu mkubwa kwa wakulima ambao hapo awali walitegemea umeme wa gridi au mafuta ya dizeli.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia ya mwaka 2021, sekta ya nishati ya umeme jua inaendelea kukua kwa kasi nchini Tanzania, lakini bado kuna changamoto zinazokabili wakulima, hasa wakulima wadogo.

Changamoto hizo zinajumuisha gharama za awali za ununuzi wa vifaa vya umeme jua na upatikanaji wa msaada wa kifedha.

Benki ya Dunia ilionyesha kuwa asilimia 60 ya wakulima wadogo walishindwa kupata ufadhili wa awali wa kununua vifaa hivyo, ingawa inaonesha kuwa mipango ya mikopo na ruzuku kwa ajili ya teknolojia ya umeme jua inaanza kuimarika.

Serikali imechukua hatua kadhaa ili kuwawezesha wakulima kutumia nishati ya umeme jua.

Kupitia mpango wa Serikali wa Umeme Vijijini, zaidi ya vijiji 100 vimewekewa vifaa vya umeme jua mwaka 2023.

Aidha, taasisi binafsi kama Shirika la Nishati Mbadala Tanzania (TAREA) zimeshirikiana na benki kutoa mikopo nafuu kwa wakulima ili waweze kumudu gharama za vifaa vya umeme jua.