Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AFCON 2025 yaweka rekodi mpya

Muktasari:

  • Fainali ya AFCON 2025 itachezwa Jumapili, Januari 18, 2025 baina ya wenyeji Morocco na Senegal na kesho Jumamosi, Januari 17, 2025 kutakuwa na mechi ya kuwania mshindi wa tatu kati ya Misri na Nigeria.

Dar es Salaam. Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zinazoendelea Morocco zimeandika historia mpya ya kuwa fainali zenye idadi kubwa zaidi ya mabao katika historia ya mashindano hayo kutokana na mabao 120 yaliyofungwa hadi sasa, kabla ya mechi za kuwania mshindi watatu na fainali mwishoni mwa wiki hii.

Idadi hiyo ya kihistoria imevunja rekodi ya awali ya mabao 102 iliyowekwa kwenye mashindano ya mwaka 2019 nchini Misri, na inaonesha dhamira ya kushambulia, ubora wa kiufundi na kuongezeka kwa kujiamini kwa timu barani Afrika.

Nyota wa Misri, Mohammed Salah akimpokonya mpira Sadio Mane wa Senegal wakati wa mechi ya robo fainali AFCON 2026.

Miongoni mwa nyota waliotoa mchango mkubwa katika rekodi hiyo ya ni nyota wa Real Madrid, Brahim Diaz anayechezea Morocco ambaye anaongoza chati ya wafungaji akiwa na mabao matano.

Anamfuatia kwa karibu ni Mohamed Salah wa Misri na Victor Osimhen wa Nigeria, kila mmoja akiwa na mabao manne.

Mshambuliaji wa Nigeria, Victoer Osimhen na Ademola Lookman wakishangilia moja ya bao katika mechi ya AFCON. Picha na Mtandao

Osimhen na Salah wanaweza kumfikia au kumpiku Diaz kwa vile timu zao zina mechi moja ya kuwania mshindi wa tatu ingawa morocco nayo ipo katika hatua ya fainali.

Rekodi ya awali iliyowekwa katika fainali za Misri 2019 ilivunjwa hata kabla ya mashindano kufikia hatua za maamuzi, huku raundi za mtoano zikiendeleza kasi hiyo badala ya kuipunguza.

Wachezaji wa Morocco, Ayoub El Kaabi na Brahim Diaz wakishangilia. Picha na Mtandao


Viwanja vya Morocco, vilivyojaa rangi, kelele na nishati, vimeonekana kutengeneza mazingira muafaka kwa mabao kufungwa na shangwe kusikika kuanzia Tangier hadi Rabat. 

Zaidi ya takwimu tu, rekodi ya mabao 120 inaakisi mabadiliko mapana katika soka la Afrika.

Mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane na Iliman Ndiaye wakishangilia baada ya kuifunga Misri katika mchezo wa robo fainali AFCON. Picha na Mtandao

Wachezaji sasa wana uhodari mkubwa wa mbinu, maandalizi bora ya kimwili na uhakika wa kiufundi, huku timu zikizidi kuwa tayari kucheza kwa mtazamo wa kushambulia.

Fainali ya AFCON 2025 itachezwa Jumapili, Januari 18, 2025 baina ya wenyeji Morocco na Senegal na kesho Jumamosi, Januari 17, 2025 kutakuwa na mechi ya kuwania mshindi wa tatu kati ya Misri na Nigeria.