Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al Ahly kuibeba Yanga Ligi ya Mabingwa

Muktasari:

  • Ahly inaongoza msimamo wa kundi D ikiwa na pointi tano sawa na Yanga huku Medeama ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne sawa na Belouizdad inayoshika mkia.

Dar es Salaam. Yanga inaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika endapo Al Ahly itapata ushindi ugenini huko Algeria leo Ijumaa Februari 16, 2024 dhidi ya CR Belouizdad.

Mchezo huo ni wa kiporo na utachezwa kuanzia saa 4:00 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki katika Uwanja wa Julai 5, 1962 jijini Algiers, Algeria.

Ikiwa Al Ahly itapata ushindi basi itajihakikishia kufuzu robo fainali lakini, itaifanya Yanga ihitaji kushinda tu mechi yake ijayo dhidi ya Belouizdad ili nayo isonge mbele.

Kama Belouizdad ikifungwa leo, itabaki na pointi zake nne na Yanga ikishinda dhidi itafikisha pointi 8 ambazo hazitoweza kufikiwa na timu hiyo ya Algeria hata kama Yanga itapoteza mechi ya mwisho dhidi ya Al Ahly.

Matokeo ya sare katika mechi ya leo, yataipa ugumu Yanga kwani yataifanya Belouizdad kufikisha pointi tano sawa nao huku Ahly wakifikisha sita na hapo kuilazimisha Yanga kuvuna pointi angalau nne katika mechi zitakazofuata dhidi ya Belouizdad na Ahly ili iweze kusonga mbele.

Refa kutoka Rwanda, Samuel Uwikunda ndiye amepangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha mechi hiyo.

Mwamuzi huyo atasaidiwa na Wanyarwanda wenzake Diedonne Mutuyimana na Eric Mugabo.

Ikumbukwe kwamba Uwikunda hivi karibuni alikuwepo Ivory Coast kuchezesha fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) ambapo, alipangwa kushika kipyenga katika mechi mbili: Guinea Ikweta na Guinea Bissau na nyingine ni ile Namibia na Mali.

Katika mechi ya kwanza ambayo ilizikutanisha Al Ahly na Belouizdad huko Cairo, Misri, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.