Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta ashinda tuzo ya Kocha Bora EPL

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Arsenal imemaliza msimu wa 2025/2026 ikiwa bingwa wa Ligi Kuu England (EPL) msimu huu.

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta ameshinda tuzo ya Meneja Bora wa Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2025/2026.

Arteta ametangazwa jana Jumanne, Mei 26 katika hafla ya utoaji wa tuzo hiyo iliyofanyika London, England.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Arteta kushinda tuzo hiyo tangu alipoanza kuinoa Arsenal mwaka 2019.

Ushindi huo kwa Arteta umekuja siku chache baada ya kuiongoza Arsenal kutwaa taji la EPL ambalo ni la kwanza kwa timu hiyo tangu ilipofanya hivyo miaka 22 iliyopita.

Pia Arteta amekuwa meneja wa kwanza kupata ushindi wa tuzo ya Meneja Bora wa msimu kwenye EPL tangu Arsene Wenger alivyofanya hivyo msimu wa 2003/2004.

Pia amekuwa meneja wa kwanza kushinda tuzo hiyo akiwa meneja wa timu aliyowahi kuichezea.

Umekuwa msimu bora kwa Arsenal chini ya Arteta ambapo imetwaa ubingwa wa EPL baada ya kukusanya pointi 85.

Timu hiyo imeruhusu mabao 27 tu ambayo ni machache zaidi huku pia ikimaliza msimu ikiww haijaruhusu penalti wala kupata kadi nyekundu.

Arteta ameibuka mshindi akiwapiku mameneja wengine watano akiwemo Pep Guardiola wa Manchester City.

Walioangukia pua mbele ya Arteta ni Keith Andrews wa Brentford, Michael Carrick (Manchester United), Pep Guardiola (Man City), Andoni Iraola (Bournemouth) na Regis Le Bris (Sunderland).