Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern yaweka rekodi ikiichapa Club Brugge

Muktasari:

  • Harry Kane amefunga bao lake la 20 msimu huu katika mechi yake ya 12 wakati Bayern Munich ikiichapa Club Brugge kwa kishindo na kuendeleza rekodi yao ya ushindi wa asilimia 100 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Kuna rekodi mbili zimewekwa katika mechi ambayo Bayern Munich imeikanda Club Brugge mabao 4-0 iliyofanyika Allianz Arena, Ujerumani usiku wa Oktoba 22, 2025.

Harry Kane amefunga bao lake la 20 msimu huu katika mechi yake ya 12 wakati Bayern Munich ikiichapa Club Brugge kwa kishindo na kuendeleza rekodi yao ya ushindi wa asilimia 100 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Nahodha huyo wa Uingereza, dakika ya 14 alifunga moja ya mabao rahisi zaidi katika maisha yake, baada ya kuachwa bila ulinzi na kutia mpira wavuni kufuatia krosi ya Konrad Laimer.

Si Lionel Messi wala Cristiano Ronaldo aliyewahi kufikia mabao 20 kwa haraka kwa mechi 12 tu.

Bao hilo la Kane lilifuatia bao la kuvutia lililofungwa na chipukizi Lennart Karl dakika tisa. Karl, mwenye umri wa miaka 17 na siku 242, aligeuka kuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga bao kwa Bayern katika historia ya Ligi ya Mabingwa, akivunja rekodi ya Jamal Musiala kwa tofauti ya siku 121.

Katika mechi yake ya kwanza kuanza, Karl alipiga shuti kali kwa mguu wa kushoto na kutikisa nyavu kwenye kona ya juu ya goli baada ya kuwapiga chenga mabeki wawili.

Luis Díaz aliongeza bao la tatu kwa shuti lililogonga mtambaa wa panya dakika ya 34, likiwa ni bao lake la saba tangu ajiunge na Bayern kutoka Liverpool majira ya kiangazi, kabla Kane hajaupiga mwamba akiwa kwenye pembe ngumu muda mfupi kabla ya mapumziko.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, alipoteza nafasi nyingine ya wazi mapema kipindi cha pili baada ya kudakwa na kipa wa Brugge, Nordin Jackers, alipokuwa uso kwa uso naye.

Kane pia alinyimwa bao la wazi baada ya kuokolewa kwa jitihada kubwa na beki Jorne Spileers, kabla ya kufanyiwa mabadiliko dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika na nafasi yake kuchukuliwa na Nicolas Jackson.

Straika huyo wa Senegal alifunga bao la nne la Bayern kutoka karibu na goli dakika chache baadaye, akihakikisha ushindi wa tatu mfululizo katika mashindano hayo, baada ya Díaz kuokolewa mpira wake uliokuwa ukielekea wavuni.

Bayern sasa wamepanda hadi nafasi ya pili nyuma ya Paris Saint-Germain katika msimamo wa hatua ya ligi, wakiwa na alama tisa sawa lakini wakiwa nyuma kwa tofauti ya mabao, huku Brugge wakishika nafasi ya 20 wakiwa na alama tatu.

Novemba 4, 2025, mabingwa hao wa Ujerumani watasafiri kwenda Ufaransa Novemba kumenyana na PSG, wakati Club Brugge watakuwa wenyeji wa Barcelona siku inayofuata.