Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fadlu aaga rasmi Simba, kocha mpya aanza kusakwa

Muktasari:

Fadlu Davids alijiunga rasmi na Simba, Julai mwaka jana akitokea raja Casablanca ambako alikuwa kocha msaidizi.

Dar es Salaam. Fadlu Davids amefunga rasmi ukurasa wake na Simba baada ya leo, Septemba 22, 2025 kuiaga rasmi klabu hiyo huku akijiandaa kukamilisha mcjakato wake wa kujiunga na Raja Casablanca ya Morocco.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Davids ameishukuru klabu hiyo na kuiombea heri katika maisha yake ya siku za usoni.

"Ni kwa moyo mzito naiaga Simba SC. Tangu nilipowasili, nilihisi shauku ya klabu hii kubwa na upendo wa mashabiki wake wa ajabu. Pamoja tulipigana, tukasherehekea na tukaimarika kupitia kila ushindi na kila changamoto. Shukrani zangu za dhati kwa Rais MO Dewji kwa uongozi wake wa kutia moyo, maono na usaidizi wake wa kudumu.

"Kwa wachezaji, endelea kupigana, endelea kuamini, na endelea kuinua beji kwa heshima.

Kwa wafanyAkazi na wasimamizi, asante kwa uaminifu wako na kujitolea bila kuchoka nyuma ya pazia.

"Kwa mashabiki wa Simba, nyinyi ndio mapigo ya moyo wa klabu hii. Sauti zenu, nyimbo zenu, shauku yenu isiyoyumba itasikika katika kumbukumbu zangu. Asante kwa kuikaribisha familia yangu kuwa yenu. Simba daima itakuwa sehemu yangu na ninaitakia klabu mafanikio na vikombe mbeleni. Asanteni Sana, forever Nguvu Moja," amesema Fadlu Davids.

Davids ameondoka Simba akiwa ameitumikia Simba kwa siku 444 tangu alipojiunga nayo Julai mwaka jana akitokea Raja Casablanca ambayo anarejea tena.

Davids anaondoka Simba akiacha kumbukumbu ya kuifikisha katika hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo walipoteza dhidi ya RS Berkane ya Morocco kwa kichapo cha jumla cha mabao 3-1, ikifungwa mabao 2-0 ugenini na kutoka sare ya bao 1-1 nyumbani.

Katika mashindano ya ndani, Davids jambo pekee analojivunia nalo ni kuiongoza Simba kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita huku akiiongoza kuishia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB ambayo ilifungwa mabao 3-1 na Singida Black Stars.

Unyonge dhidi ya Yanga pengine ni kumbukumbu mbaya ambayo Fadlu Davids anaiacha Simba ambapo katika mara nne alizokutana na timu hiyo, alipoteza zote ambapo mbili ni kwenye Ligi Kuu na mechi mbili ni za Ngao ya Jamii.

Kwenye mechi hizo zote ambazo Simba chini ya Fadlu Davids imepoteza dhidi ya Yanga, haikufunga bao lolote huku ikiwa imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara tano.

Wakati Fadlu Davids akiiaga Simba, chanzo kutoka ndani ya klabu hiyo kimefichua kuwa tayari imeshaanza kutafuta mrithi wake.

"Suala la kutafuta kocha mpya litafanyika kwa haraka kwa sababu muda uliobakia kabla ya mechi ya marudiano na Gaborone United ni mfupi na timu inahitaji kuwa na msimamizi wa benchi la ufundi mapema kabla msimu haujaanza kuchanganya," kilifichua chanzo hicho.