Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali ya heshima, noti Mapinduzi

Muktasari:

  • Timu itakayotwaa taji hilo maana yake itaandika historia ya kuwa ya kwanza kutwaa ubingwa katika muundo mpya wa mashindano hayo ambao unashirikisha timu za taifa tofauti na klabu lakini itapata kiasi cha Sh100 milioni za zawadi ya bingwa.

Pemba. Zanzibar Heroes na Burkina Faso leo kila moja ina nafasi ya kaundika historia ya heshima huku ikibeba noti iwapo itafanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi katika fainali itakayochezwa leo kuanzia saa 2:00 usiku katika Uwanja wa Gombani.

Timu itakayotwaa taji hilo maana yake itaandika historia ya kuwa ya kwanza kutwaa ubingwa katika muundo mpya wa mashindano hayo ambao unashirikisha timu za taifa tofauti na klabu lakini itapata kiasi cha Sh100 milioni za zawadi ya bingwa.

Ni mara ya pili timu hizo kukutana baada ya awali kuvaana katika mechi ya makundi na wageni kushinda kwa bao 1-0, hivyo leo ni zamu ya wenyeji kujitutumua na kulipa kisasi.

Timu nne za mataifa ya Kenya, Burkina Faso, Tanzania Bara na Zanzibar ndio zilizoshiriki hatua ya awali baada ya nchi za Uganda na Burundi kuchomoa dakika za mwishoni, ambapo Burkina Faso ilimaliza kinara wa msimamo ikivuna pointi saba, mabao manne ya kufunga na kufungwa moja katika mechi tatu.

Mwenyeji Zanzibar ilimaliza ya pili katika msimamo ikiwa na pointi sita kupitia mechi tatu pia, ikishinda michezo miwili na kupoteza moja, ikifunga mabao mawili na fungwa moja, mbele ya Kenya iliyomaliza ya tatu kwa alama nne, huku Kilimanjaro Stars ya Bara ikiburuza mkia bila pointi wala bao lolote.

Katika mchezo huo Zanzibar itaendelea kumtegemea nahodha, Feisal Salum 'Fei Toto' mwenye bao moja na asisti moja vilevile katika kuhakikisha inalibakiza taji hilo visiwani Zanzibar ili kunogesha sherehe za Siku ya Mapinduzi iliyoadhimishwa jana Jumapili ikiwa ni miaka 61 tangu yalipofanyika Januiaru 12, 1964.

Mbali na Fei Toto, timu hiyo ya Zanzibar itakayomkosa beki wa kati Ibrahim Ame aliyelimwa kadi nyekundu katika mechi iliyopita dhidi ya Kenya, itawategemea pia Ibrahim Hamad 'Hilika', Maabad Maulid, Khatib Idd 'Gego' na wengine kuwabana Burkina Faso wanaomtegemea zaidi Clément Pitroipa.

Nyota huyo wa Burkina Faso ndiye kinara wa mabao kwa sasa wa michuano hiyo akifunga mawili alipoizamisha Kilimanjaro Stars kwa mabao 2-0, lakini ina mastaa wengine wenye vipaji ambao wanafaa kuchungwa kama wenyeji wanataka kulibakiza kombe na fedha hizo za Mapinduzi 2025.

Haitakuwa mechi rahisi kwa timu zote kutokana na aina ya soka lililochezwa kwenye mechi za hatua ya awali, lakini Zanzibar Heroes ikiwa na kazi kubwa ya kuwazuia Waburkinabe ambao wanacheza soka la kasi na la nguvu, ili kuweka heshima mbele ya Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi wa fainali hiyo.