Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Filamu za Afrika Mashariki ndani ya tuzo za Tanzania

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini (TFB), Dk Kiagho Kilonzo

Muktasari:

  • Bodi ya Filamu nchini (TFB), imetangaza kufungua msimu wa tatu wa tuzo za filamu, ambapo wameongeza kipengele kimoja kipya cha ‘Filamu bora ya Afrika Mashariki.’

Dar es Salaam. Bodi ya Filamu nchini (TFB), imetangaza kufungua msimu wa tatu wa tuzo za filamu, ambapo wameongeza kipengele kimoja kipya cha ‘Filamu bora ya Afrika Mashariki.’

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa maendeleo ya filamu wa bodi hiyo, Emmanuel Ndumukwa, alipokuwa akitangaza uzinduzi wa msimu wa tatu wa utoaji wa tuzo hizo.

Amesema kazi hizo zitakazoanza kupokelewa kuanzia Agosti 11, 2023 na dirisha litafungwa Septemba 25, 2023, zitafanya vipengele vitakavyoshindaniwa kuwa 32, kutoka 31 zilizoshindaniwa mwaka jana.

Mratibu wa tuzo hizo, Rachel Mng’ong’o, alivitaja vigezo anavyopaswa kuwa navyo mshiriki ni pamoja na kazi lazima iwe na hakimiliki za muhusika, kuwa na nakala ya leseni, kitambulisho cha taifa, kitambulisho cha mpiga kura au hati ya kusafiria.

Kigezo kingine ni kazi lazma iwe imeandaliwa na mtanzania, filamu iwe katika mfumo wa HD na katika muundo wa MP4 au MOV.

Alizitaja filamu zinazopaswa kuwasilishwa kuwa ni pamoja na tamthilia, filamu fupi, filamu ndefu, filamu za ucheshaji, makala na animation na ziwe zilizotoka kuanzia Juni 2022 hadi Agosti 2023; na kwamba kwa upande wa tamthiliya, mshiriki atapaswa kuwasilisha episode tatu zinazofuatana.

Aidha kwa filamu za Afrika Mashariki, Rachel amesema filamu lazma ziwasilishwe kupitia mtandao wa feel free way, izungumze asilimia 50 ya lugha ya kiswahili, au subtitle ya Kiswahili pale ambapo kumetumika lugha nyingine.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa TFB Dk Kiagho Kilonzo, amesema tangu tuzo hizo zimeanza, zimekuwa za mafaniko kwani wasanii washindi wamekuwa wakipata kazi za ndani na nje, ambapo amesema tuzo hizo ni jukwaa pia la watayarishaji filamu kutangaza kazi zao.

Baadhi ya wasanii waliozungumzia tuzo hizo, akiwemo Yvonne Cherrie ‘Monalisa’, amesema ameipongeza bodi hiyo na kusema amependa mwaka huu wameshirikisha filamu ya Afrika Mashariki, kwani itawasaidia kuona wenzeo wanafanya nini na wao wanafanya nini ili kuacha kujikita katika ushindani wa ndani kuangalia nchi za wengine.

Kwa upande wake, Jacline Wolper, amesema akiwa balozi wa bodi ya filamu wanamfanya ajiamini mbele za watu kwani wanafanya kazi nzuri zinazoonekana na kuwataka wasanii kuendelea kushirikana nao kwa karibu ili kuijenga tasnia ya filamu nchini.