Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya hapa matokeo ya mpira wa wavu Umitashumta Iringa

Muktasari:

  • ‎Mashindano ya UMITASHUMTA upande wa mpira wa wavu yameanza leo Juni 11, 2025 katika viwanja vya chuo cha Ualimu Kleruu halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambapo mchezo upande wa wanaume, timu ya mwenyeji Iringa iliibuka na ushindi wa seti 3-1 dhidi ya Kagera huku ikibeba hisia za mashabiki ambao wanajitokeza katika viwanja hivyo kushuhudia michezo hiyo.

Iringa. Mashindano ya mpira wa wavu ya UMITASHUMTA 2025 yameendelea kushika kasi katika viwanja vya chuo cha Ualimu Kleruu mkoani Iringa, huku wenyeji wa mashindano hayo, timu ya wasichana ya Iringa, ikiipa sababu ya kutabasamu hadhira ya nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3-1 dhidi ya Kagera.

‎Iringa walionyesha mchezo wa kuvutia na kujiamini, wakishinda seti ya kwanza kwa ustadi mkubwa. Kagera walijaribu kujibu mapigo kwa kuchukua seti ya pili, lakini Iringa walijipanga upya na kuendeleza ubabe wao kwa kuchukua seti mbili zilizofuata, na hivyo kutwaa ushindi wa jumla wa 3-1.

‎Michezo hiyo imepigwa Leo Juni 11, 2025 katika viwanja vya Kleruu, mkoani Iringa, ikihusisha mpira wa wavu kwa wasichana na wavulana kutoka shule za mikoa mbalimbali nchini katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) 2025 yanayoendelea mkoani Iringa.

‎Katika mchezo wa mpira wa wavu kwa wasichana, timu ya Mtwara ilianza kwa kishindo kwa kuichapa Lindi seti 3-1, ambapo Mtwara walichukua seti ya kwanza, Lindi wakasawazisha kwa kushinda seti ya pili, lakini Mtwara walirejea kwa nguvu na kushinda seti mbili zilizofuata, kuibuka na ushindi wa jumla wa 3-1.

‎Katika michezo mingine ya mpira wa wavu kwa wasichana, Kilimanjaro iliifunga Pwani seti 3-0, Dar es Salaam iliichapa Simiyu seti 3-0, Tanga iliifunga Tabora seti 3-0, na Dodoma iliichapa Arusha seti 3-0.

‎Kwa upande wa wavulana, Kilimanjaro iliifunga Tabora seti 3-0, na Mtwara iliichapa Arusha seti 3-0.

‎Michezo hii ya UMITASHUMTA imeanza rasmi jana Juni 10, 2025 kwa kuchezwa michezo mbalimbali katika viwanja vya Kichangani, Kleruu, gangilonga na Iringa Girls mkoani Iringa na inatarajiwa kumalizika Juni 17, 2025.