Hispania yaitupa nje Uruguay
Muktasari:
- Bao la Alex Baena dakika ya 42 limetosha kuipa Hispania ushindi huo akipokea pasi nzuri kutoka kwa Marcos Llorente.
Hispania imefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kuichapa Uruguay kwa bao 1-0 na kuitupa nje ya mashindano timu hiyo.
Bao la Alex Baena dakika ya 42 limetosha kuipa Hispania ushindi huo akipokea pasi nzuri kutoka kwa Marcos Llorente.
Kipa wa Uruguay, Fernando Muslera atajilaumu mwenyewe kwani kabla ya kuingia kwa bao hilo, alishidwa kuzuia mpira huo aliougusa na kupita mikononi mwake.
Mpaka mapumziko, Hispania ilitoka ikiongoza kwa bao hilo huku ikitawala vizuri kipindi hicho cha kwanza mbele ya Uruguay.
Kipindi cha pili, Uruguay ikaja juu ikitaka kusawazisha bao hilo lakini kizuizi kikawa kipa wa Hispania, Unai Simon ambaye alifanya kazi nzuri kuokoa mashambulizi mawili.
Wakati mchezo huo ukielekea mwisho, Uruguay ilipata pigo baada ya nyota wake, Agustin Conobio kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kucheza faulo mbaya dakika ya 90+5.
Ushindi huo wa Hispania umeifanya imalize ikiongoza kundi H ikifikisha pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja, wakati Uruguay ikitupwa nje kwa kumaliza nafasi ya tatu ikikusanya pointi mbili.