Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hojlund afunguliwa mlango wa kuondoka Man United

Muktasari:

  • United walikuwa wakisaka mshambuliaji wa kati kwa muda mrefu baada ya chaguo lao la kwanza, Liam Delap, kujiunga na Chelsea, huku Hugo Ekitike na Viktor Gyokeres wakihamia Liverpool na Arsenal mtawalia.

Manchester United wameripotiwa kuwa tayari kumruhusu mshambuliaji Rasmus Hojlund kuondoka katika dirisha hili la usajili, baada ya kukamilisha dili la kumsajili Benjamin Sesko kutoka RB Leipzig.

Kwa mujibu wa Gazzetta Dello Sport, AC Milan wanavutiwa kumsajili Hojlund ikiwa ataruhusiwa kuondoka kwa mkopo, na wanataka makubaliano hayo yawe na kipengele cha kumnunua moja kwa moja. Hii ingewapa nafasi ya kulipa ada ya uhamisho kwa awamu badala ya kutoa fedha zote msimu huu wa kiangazi.

Hojlund amefunga mabao 26 katika mechi 95 tangu ajiunge na United akitokea Atalanta majira ya kiangazi mwaka 2023. Uwezekano wa kurejea Serie A unakuja huku Sesko akikaribia kutoka Bundesliga.

Ripoti za Daily Mail Sport zinaeleza United wamekubaliana na Leipzig ada ya awali ya pauni milioni 66.4, pamoja na nyongeza za pauni milioni 7.4. Newcastle walitoa dau kubwa zaidi, lakini mchezaji alipeleka mapenzi yake Old Trafford, jambo lililosaidia dili kukamilika haraka wiki hii.

Tangu ahamie Ujerumani kutoka Red Bull Salzburg, Sesko amefunga mabao 39 na kutoa pasi 8 za mabao katika mechi 87.

United walisalia kimya wakati wote wa mbio za kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Slovenia, wakiacha Newcastle waanze mazungumzo mapema. Newcastle walijaribu mara mbili kumchukua kabla ya United kuingia rasmi kwenye ushindani Jumanne.

Kaskazini Mashariki, Sesko alikuwa akionekana kuwa mrithi wa Alexander Isak, ambaye anataka kujiunga na Liverpool majira haya ya kiangazi. Hata hivyo, Liverpool tayari wamekataliwa ofa ya pauni milioni 110 kwa Isak, na huenda wasirudi na dau kubwa zaidi hadi pale Newcastle watakapompata mshambuliaji mpya.

United walikuwa wakisaka mshambuliaji wa kati kwa muda mrefu baada ya chaguo lao la kwanza, Liam Delap, kujiunga na Chelsea, huku Hugo Ekitike na Viktor Gyokeres wakihamia Liverpool na Arsenal mtawalia.