Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyu ndiyo Rachid Taoussi, kocha mpya wa Azam Fc

Enzi za uchezaji wake alikuwa kiungo mchezeshaji, yaani namba 10, akianza kucheza 1977 kwenye klabu ya Sid Kacem iliyobeba jina la kitongoji alichozaliwa.

Baada ya kufungwa kwa ukurasa wa Yousouph Dabo kwenye viunga vya Azam Complex, sasa umefunguliwa ukurasa mpya wa Rachid Taoussi, kocha kutoka Morocco.

Ukurasa huu unakuletea uchambuzi wa kina kumjua vizuri kocha huyu mkongwe.


1. Mkongwe kweli kweli

Alizaliwa 26 Februari, 1959 kwenye kitongoji cha Sidi Kacem cha jiji la Rabat, nchini Morocco.

Enzi za uchezaji wake alikuwa kiungo mchezeshaji, yaani namba 10, akianza kucheza 1977 kwenye klabu ya Sid Kacem iliyobeba jina la kitongoji alichozaliwa.

Alidumu hapo kwa misimu minane, hadi 1986 alipohamia timu ya jeshi la Morocco ya FAR Rabat anbayo alidumu nayo msimu mmoja tu 1987, akastaafu kucheza na kuhamia ukocha.

Kama kocha, ni muumini mkubwa wa soka la pasi nyingi na za haraka haraka kwenda kwenye lango la mpinzani.

Alianza kufundisha soka tangu mwaka 1991 kwenye klabu ya mji aliozaliwa na kukulia wa Sidi Kacem.

Kutoka hapo akafundisha timu za vijana za Morocco, akawa mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho la soka la kiflame la Morocco na akafundisha vilabu kadhaa hasa vikubwa kama Wydad na Raja, vya jijini Casablanca.

Pia amefundisha timu ya taifa ya Morocco kwa vipindi viwili, ikiwemo mwaka 2014 alipokutana na kipigo cha 3-1 kutoka Taifa Stars.


2. Kocha wa makombe

Kama Azam FC shida yao ni makombe basi kwa kocha huyu watayapata.
Rachid Taoussi ni kocha aliyeshinda mataji mengi kama kocha, kama mkurugenzi wa ufundi na kama menaja mkuu. Jumla ameshinda mataji 9
Ameshinda mataji manne akiwa kama kocha kwenye timu kadhaa, lakini taji kubwa zaidi ni Kombe la Shrikisho la CAF aliloshinda mwaka 2011 akiwa na klabu ndogo ya Morocco ya Magharib Sportive de Fes (MAS).

Ubingwa huu ukampatia nafasi ya kucheza mechi ya CAF Super Cup mwaka 2012 na kushinda.

Mwaka 1997 akiwa bado kocha mchanga, alishinda AFCON ya vijana chini ya mioaka 20 wakiwa na timu ya taifa ya Morocco.
Pia ameshinda mataji kadhaa nchini UAE akiwa na klabu ya Al Ain. 


3. Kocha wa Afrika

Zaidi ya makombe, Azam FC inateseka sana kutoboa kwenye mashindano ya Afrika.

Kama watamtumia vizuri, Rachid Taoussi ni kocha mwenye #Code za Afrika.
Ukiacha ubingwa wa Kombe la Shirikisho mwaka 2011 akiwa na MAS, kocha Taoussi ameshafika mara kadhaa hatua za makundi, robo fainali na nusu fainali za mashindano ya Afrika akiwa na Berkane, Raja na Wydad.


4. Kocha la 'boli kutembea'

Rachid Taoussi ni kocha mzuri sana kimbinu mwenye kupenda kuliacha boli litembee kwa staili ya tikitaka, akiwa muumini mkubwa sana wa Pep Guardiola.

Timu yoyote ambayo ameifundisha husifika kwa kuweka mpira chini siyo kubutua.

Mara zote anataka kukaa na mpira huku akimfanya mpinzani ahangaike kumkaba, siyo yeye kukaba kaba.

Ili kuyafikia haya, ni lazima timu ifanye mazoezi magumu na yamuda mrefu, na hiyo ndiyo sifa yakle nyingine.
Rachid hufanya mazoezi na timu yake kwa vipindi viwili kwa siku, asubuhi na jioni.


Madhaifu yake

Hakuna kilicho bora kisicho na kasoro, na kocha Taoussi hali kadhalika.


1. Kocha 'mkorofi'

Alipokuwa Raja, Taoussi aligombana sana na wachezaji kutokana na ukali wake.

Hata hivyo, migogogro yake na wachezaji mara zote ni katika kujenga, siyo kubomoa.

Kwa mfano, ugomvi wake na wachezaji wa Raja ulikuwa kwa ajili ya matokeo.
Timu isiposhinda, au ikishinda lakini siyo kwa kucheza kama alivyoagiza yeye, basi siku inayofuata ni mazoezi magumu.

Alifanya hivi ili kuwafanya wachezaji siyo tu washinde mechi bali kwa kufuata maelekezo yake.

Hili lilisababisha migogoro ya hapa na pale kati yake na wachezaji ambao waliishi kwenye 'comfort zone' yaani walibweteka.


2. Dhaifu kuusoma mchezo

Taoussi ni kocha mwenye tatizo kubwa sana katika kuusoma mchezo wakati ukiendelea.

Kwa maana kwamba hupata tabu kugundua tatizo la timu yake inapokuwa katika wakati mgumu kwenye mchezo.

Kuepuka hili, mara zote huwa na msaidizi mzuri mwenye uwezo mkubwa kufidia mapungufu ya kocha.

Na hata sasa amemchagua Eddine Drissi kuwa msaidizi wake. Huyu ni kocha mkubwa pia na ni mchambuzi wa TV kubwa sana huko Dubai.

Alikuwa kocha msaidizi wa Wydad ilipofika fainali ya African Football League na kupoteza kwa Mamelod Sundowns.


3. Anapenda 'mahewa'

Rachid ni kocha anayependa sana kuonekana kwenye vyombo vya habari Kama kuna kipindi ambacho waandishi wa habari Tanzania watafurahia kazi yao ni hiki.


Wasifu wake

2022 = Kocha mkuu Raja 
Robo fainali ligi ya mabingwa
Makamu bingwa ligi kuu

2020 - 2020 = Meneja wa maendeleo ya mpira wa shirikisho la soka la Morocco na mshauri wa Rais wa shirikisho.

2019 = Kocha mkuu wa OCK (Olympique Club de Khouribga) ya Morocco
2018 = Kocha Mkuu ESS (Entente Sportive Setifienne) ya Algeria.


Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa

2017 = Kocha mkuu wa CRB (Chabab Rhyadi Belouizidad) ya Algeria.

2016/17 = Kocha mkuu RS Berkane ya Morocco 

2015 - 2017 = Mjumbe wa shirikisho la soka la Morocco

2014/15 = Kocha mkuu Raja 

2013/14 = Kocha mkuu FAR Rabat

2012/13 = Kocha mkuu timu ya taifa ya Morocco

2010 - 2012 = Kocha mkuu MAS

Bingwa wa kombe la mfalme (sawa na FA Cup)

Bingwa kombe la shirikisho la CAF


Bingwa wa CAF Super Cup

2008 - 2010 = Meneja mkuu Al Ain - UAE

2007 - 2008 = Kocha mkuu MAS

2007 = Kocha mkuu FUS Rabat

2004 - 2007 = Mkurugenzi wa ufundi wa Al-Shabab Al-Arabi Club ya Dubai.

2003 - 2004 = Mkurugenzi wa ufundi wa Wydad Athletic club (WAC) ya Morocco.

2000 - 2002 = Mkurugenzi wa ufundi shirikisho la soka la Morocco.

1999 - 2000 = Kocha mkuu FAR rabat.

1997 - 1998 = Kocha msaidizi timu ya taifa ya Morocco chini ya Microsoft Word - Henri Michel (Kombe la dunia 1998).

1995 - 1997 = Kocha mkuu timu ya taifa ya Morocco chini ya miaka 20.

1993 - 19975= Timu ya taifa ya Morocco chini ya miaka 16.

1991 - 1993 = Kocha mkuu wa Sidi Kacem FC.

Karibu Tanzania Kocha Rachid Taoussi.