Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ipswich Town wataiweza mikiki ya EPL

Baadhi ya mashabiki wa Ipswitch Town wakishangilia ndani ya uwanja wa Portman Road baada ya kurejea Ligi Kuu England. Picha na ,Mtandao

Muktasari:

  • pswich wamefanya mabadiliko makubwa msimu uliopita kwa kusajili wachezaji 11 wapya miongoni mwao alikuwa kiungo mshambuliaji wa Chile, Marcelino Nunez, aliyesajiliwa kutoka Norwich kwa paundi milioni 10.

London, England. Umekuwa msimu mzuri kwa mashabiki wa Ipswich Town, ambao waliiona timu yao ikiifunga mara mbili Norwich City katika derby za East Anglia, na pia bila kusahau kupanda daraja kurejea Premier League.

Baadhi wanaweza kusema kupanda daraja mwaka 2024 ilikuwa mafanikio makubwa zaidi, hasa ikizingatiwa kuwa timu hiyo ilikuwa imepanda kutoka League One miezi 12 tu kabla yake.

Wengine wanaweza kuamini kuwa kurejea baada ya kushuka daraja msimu uliopita na kuirudisha klabu kwenye mstari sahihi ni ushahidi mkubwa zaidi wa uwezo wa ukocha wa Kieran McKenna.

Baadhi ya wachezaji wa Ipswitch wakishangilia moja ya bao katika mechi ya Championship dhidi ya Millwall iliyopigwa jana Mei 2, 2026. Picha na Mtandao

Kushuka daraja kulikuja baada ya ushindi mmoja tu katika mechi 19 za mwisho, lakini Muirish huyo wa Kaskazini amerejesha sifa yake msimu huu kama mmoja wa makocha chipukizi bora nchini England.

Hivi karibuni pia alitajwa kuwa mgombea wa nafasi ya ukocha katika AFC Bournemouth kabla kazi hiyo kupewa Marco Rose.

Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Ipswich, Mark Ashton, alisema: “Kieran ni meneja wa kipekee sana. Anahitajika sana na vilabu vingi vya Championship, Premier League na hata vilabu vikubwa Ulaya—yuko daraja la juu kabisa.”

Aliongeza kuwa angependa McKenna abaki klabuni hapo milele, lakini akakiri kuwa soka lina mizunguko yake na hakuna kitu cha kudumu milele.

Ashton pia alisema kuwa “klabu hii inapoungana kikamilifu, haiwezi kuzuilika,” jambo lililoonekana wazi katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Queens Park Rangers uliowahakikishia nafasi ya pili kwenye Championship.

Mahusiano kati ya uongozi wa klabu na benchi la ufundi ni muhimu sana, ingawa mara nyingi si mazuri katika baadhi ya vilabu—mfano ukiwa Tottenham Hotspur na Chelsea.

Ingawa Ashton na McKenna hawana muda wa kujumuika kijamii, ni wazi kuwa wana maelewano makubwa kazini. Ashton alisema anampa McKenna nafasi ya kufanya kazi yake huku akihakikisha anapata kila anachohitaji bila visingizio.

Ipswich walifanya mabadiliko makubwa msimu uliopita kwa kusajili wachezaji 11 wapya, wakisaidiwa na fedha za kushuka daraja. Miongoni mwao alikuwa kiungo mshambuliaji wa Chile, Marcelino Nunez, aliyesajiliwa kutoka Norwich kwa takriban pauni milioni 10.

Ilichukua muda kwa kikosi hicho kipya kuzoea pamoja, kwani hawakushinda mechi yoyote kati ya nne za mwanzo wa ligi. Lakini waliboresha kiwango kadri msimu ulivyoendelea.

Kocha McKenna alisema: “Wachezaji wamekua sana msimu huu. Hatukupata matokeo kirahisi, lakini kupanda daraja ni mafanikio makubwa sana. Kumaliza kwa kupoteza mechi moja tu kati ya 15 kunaonyesha umoja wa kikosi.”

Hata hivyo, Ipswich wana changamoto kadhaa kabla ya kurejea Premier League. Moja ni safu ya ushambuliaji hawakusajili mshambuliaji mpya Januari kuongeza ushindani kwa George Hirst na Ivon Azon. Hirst amefunga mabao ya kutosha msimu huu, lakini Azon amefunga mara tano tu.

Baadhi ya wachezaji wa Ipswitch Town wakishangilia baada ya kupanda daraja ambapo msimu ujao watashiriki Ligi Kuu England.

Msimu uliopita walifunga mabao 36 pekee katika mechi 38 za ligi kuu, hivyo ni wazi wanahitaji mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga mara kwa mara ili kubaki kwenye ligi hiyo.

Pia kuna maswali kuhusu kipa Christian Walton na uimara wa safu ya ulinzi, lakini hayo yatajadiliwa zaidi baadaye.

Msanii Ed Sheeran, ambaye pia ni mbia mdogo wa klabu hiyo, alisema: “Nina furaha kwa klabu na kwa jimbo zima inaleta matumaini na furaha kwa watu.”

Mshambuliaji wa zamani wa Ipswich, Shefki Kuqi, anaamini timu hiyo “inastahili” kuwa Premier League na ana uhakika watafanya vizuri zaidi msimu ujao kutokana na uzoefu walioupata.

Alisema: “Sasa wana uzoefu na tayari wamekuwa huko kabla, hivyo wako tayari zaidi naamini wataendelea kubaki hapo.”