Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak kuikosa mechi ya ufunguzi kisa Liverpool

Kocha wa Newcastle United, Eddie Howe, amesema anataka kuwa na wachezaji wanaotaka kweli kubaki kwenye timu, kauli inayoashiria kuuzwa kwa Alexander Isak.

Isak, raia wa Sweden, hajajiunga na mazoezi ya timu na hataichezea Newcastle kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa wiki ijayo, baada ya kueleza wazi kuwa anataka kujiunga na Liverpool.

Hata hivyo, dili hilo halitakamilika mpaka Newcastle wapate straika mbadala na mabingwa hao wa England warudi na ofa itakayokubalika. Wiki iliyopita, Newcastle walikataa ofa ya pauni milioni 110 kutoka Liverpool.

Howe amesema anapendelea Isak abadili mawazo na kusalia, lakini anakiri hilo halionekani kuwa rahisi.

“Kila kitu kiko wazi kwa sasa. Isak bado ni mchezaji wetu na mkataba wake ni mali ya klabu. Uamuzi wa mwisho utakuwa wa klabu. Ninachotaka mimi ni kuwa na kikosi bora na chenye nguvu, lakini pia na wachezaji wanaotaka kucheza kwa ajili ya klabu hii,” amesema kocha huyo wa Newcastle.

Kocha huyo alifichua kuwa baada ya mazungumzo na Isak, ilionekana wazi kwamba straika huyo hawezi kushiriki mazoezini wala kucheza mechi.

“Ninamtaka awe anafanya mazoezi nasi na kutuchezea, lakini lazima iwe sawa kutoka pande zote mbili,” aliongeza.

Hatma ya Isak ipo mikononi mwa wamiliki wa klabu hao kutoka Saudi Arabia. Ingawa msimamo rasmi ni kwamba hayupo sokoni, baadhi ya viongozi wanaona kuwa kumuuza kwa masharti yao kunaweza kuwa bora kwa manufaa ya muda mrefu ya klabu. Ndiyo maana Newcastle wamekuwa wakimfuatilia Joao Pedro, Hugo Ekitike na Benjamin Sesko kama mbadala wa straika huyo mwenye umri wa miaka 25.

Katika mechi ya kirafiki Jumamosi, Newcastle walifungwa 2-0 na Atletico Madrid, wakimaliza maandalizi ya msimu mpya bila ushindi, wakiwa na sare mbili na vichapo vinne.

Anthony Gordon, ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Isak dhidi ya Villa, alipata majeraha ya kifundo cha mguu, lakini Howe amesema atakuwa sawa.

Klabu pia imepata habari njema baada ya kukubaliana dili la pauni milioni 34.3 kumsajili beki wa AC Milan, Malick Thiaw, anayetarajiwa kufanyiwa vipimo.

Hata hivyo, kipaumbele kwa Newcastle ni kumpata straika mpya, huku Howe akikiri mashabiki wana hofu kuanza msimu bila mfungaji wa uhakika.

“Huo ni ukweli. Tunapaswa kutafuta njia za kuongeza mabao kwenye timu. Kazi ya kocha ni kujua namna ya kushinda mechi, na hilo ndilo tunalopaswa kulifanya,” amesema Howe.

Akizungumzia majira haya ya usajili yenye sintofahamu, Howe ameongeza:

“Nina mtazamo wa wastani. Hali ikionekana nzuri siyo nzuri sana kama unavyofikiria, na ikionekana mbaya siyo mbaya sana. Huu ni mtihani mpya kwetu, lakini naamini changamoto zikikabiliwa vizuri zinaweza kuleta kitu cha kipekee.”