Ivory Coast yazikimbiza Morocco, Senegal kuelekea Kombe la Dunia
Licha ya kuwa na kundi kubwa la nyota wenye majina makubwa, Morocco na Senegal zimezidiwa na Ivory Coast katika chati ya timu za Afrika zenye vikosi vya thamani kubwa zaidi kwenye Kombe la Dunia 2026.
Tathmini iliyofanywa na mtandao wa Transfermkt inaonyesha kuwa Ivory Coast ndio timu ya Afrika yenye kikosi ghali zaidi kati ya 10 zinazoshiriki Kombe la Dunia ambapo nyota wake 26 kwa jumla wana thamani ya Pauni 459.07 milioni (Sh1.6 trilioni).
Hata hivyo kwa kulinganisha na timu za mabara mengine zinazoshiriki fainali hizo, Ivory Coast inashika nafasi ya 11.
Mshambuliaji wa Morocco, Brahim Diaz. Picha na Mtandao
Timu ya taifa kutoka Afrika inayoshika nafasi ya pili kwa kuwa na kikosi chenye thamani kubwa zaidi katika Kombe la Dunia ni Morocco ambayo wachezaji wake 26 wanafanya timu hiyo kuwa na kikosi chenye thamani ya Pauni 422.15 milioni (Sh1.5 trilioni).
Inayoshika nafasi ya tatu kwa kuwa na kikosi chenye thamani kubwa katika Kombe la Dunia kwa timu za Afrika ni Senegal ambayo yenyewe kikosi chake kina thamani ya Sh1.4 trilioni.
Kiujumla katika timu 48 zinazoshiriki Kombe la Dunia, yenye thamani kubwa zaidi ni Ufaransa ambayo kikosi chake kina thamani ya
Katika vikosi hivyo, Ufaransa ndio kinara kwa kuwa na kikosi chenye thamani kubwa zaidi ambapo kina thamani ya Sh4.6 trilioni.
Nafasi ya pili inashikiliwa na kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi ambacho kina thamani ya Sh3.9 trilioni.
Hispania yenye kikosi chenye thamani ya Sh3.8 trilioni inashika nafasi ya tatu na inayoshika nafasi ya nne ni Ureno ambayo kikosi chao kina thamani ya Sh3.1 trilioni.
Katika orodha hiyo, nafasi ya tano ipo Ujerumani ambayo kikosi chake kina thamani ya Sh3 trilioni.
Timu ambayo ina kikosi chenye thamani ndogo zaidi katika Kombe la Dunia ni Jordan ambayo kikosi chake kina thamani ya Pauni 16.89 milioni (Sh59.5 bilioni).