Kisa kipigo Misri yamnyooshea kidole Refa Mfaransa
Muktasari:
- Argentina itakutana na Switzerland katika mechi ya hatua ya robo fainali itakayochezwa Julai 12, 2026.
Misri imeshambulia refa François Letexier kutoa Ufaransa ikidai amechangia itolewe katika Fainali za Kombe la Dunia 2026.
Jana, Misri ilipoteza kwa mabao 3-2 dhidi ya Argentina katika mechi ya hatua ya mtoano ya 16 Bora, matokeo ambayo Misri inadai yalisababishwa na refa Letexier.
Katika mchezo huo, Misri inadai kwamba Salah alichezewa rafu katika eneo la hatari la timu pinzani na Refa huyo hakutaka kwenda kujiridhisha katika hilo.
"Sitaki kuzungumza kuhusu refa kwa sababu nitakuwa matatizoni nikiongea. Inasikitisha na kuumiza kuona maamuzi yote yapo dhidi yako katika mechi hasa ya uamuzi kama hii kwenye Kombe la Dunia. Ni jambo baya sana katika pointi hii kwenye soka," amesema Salah ambaye ni nahodha wa timu hiyo.
Kocha Mkuu wa Misri, Hossam Hassan amesema kuwa Misri ilionewa kwa sababu za kibiashara.
"Sisi ni timu bora lakini soka sio mara zote linakuwa na usawa. Labda wanataka mabingwa wa dunia na Messi kuendelea katika Kombe la Dunia kwa malengo ya kimasoko," amesema Hassan.
Baada ya ushindi huo wa jana, Argentina sasa itakutana na Switzerland katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo, mechi iliyopangwa kuchezwa Julai 12 mwaka huu.
Katika hatua nyingine, refa Letexier amejiondoa katika kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa kile kinachoonekana kukwepa luga za matusi na vitisho ambavyo amekipewa na mashabiki wa soka kutoka maeneo tofauti duniani