Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maeneo yanayoitesa Simba

Muktasari:

Soma zaidi hapa...

Juzi Jumamosi, Simba ilikuwa Tunisia kucheza dhidi ya Esperance katika mechi ya tatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kundi D. Kabla ya mechi hiyo, Simba ilikuwa imekatiwa tamaa ya kutoboa kufuzu robo fainali msimu huu kutokana na matokeo mabaya iliyopata awali.

Kuanza kufungwa 1-0 nyumbani dhidi ya Petro Atletico, kisha kichapo cha 2-1 ugenini mbele ya Stade Malien, Simba imeonekana kuwa na mlima mrefu wa kupanda kulinda rekodi yake ya kufuzu robo fainali kina inapocheza makundi.

Hata hivyo, baada ya mechi dhidi ya Esperance na kufungwa bao 1-0, imetoa taswira halisi ya Simba inachokabiliana nacho msimu huu. Kumbuka timu hiyo kuanzia 2018 hadi 2025, imefanikiwa kucheza makundi ya michuano ya CAF mara saba na zote imetoboa kwenda robo fainali bila ya kujali imeanza vizuri au vibaya. Kwa kifupi, Simba imekuwa na rekodi ya kutoishia makundi ndani ya muda huo, lakini safari hii, ngoma ngumu.

Msimu wa 2022–2023 katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ilianza vibaya kwa kupoteza mechi mbili za kwanza, lakini ikatoboa kutokana na kushinda tatu zilizofuatia, ile ya mwisho ikapoteza, hata hivyo pointi ilizokusanya ziliwavusha kibishi.

Simba iliyocheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita, safari hii ilitazamiwa kufanya makubwa zaidi, lakini changamoto ilizopitia tangu Septemba 2025 hadi sasa, zimewaangusha kiasi cha kuonekana haina tumaini tena, huku mashabiki wa timu hiyo wakitishia kuwasusia viongozi wakidai ndiyo sababu ya haya yote kutokea.


Miezi mitatu, makocha watano

Kwa timu inayohitaji kufanya vizuri, ni nadra sana kuona ndani ya kipindi kifupi cha takribani miezi mitatu, kuna makocha watano tofauti wamefundisha. Kumbuka kila mmoja hapo aliingia kwenye mechi na mpango wake uliotakiwa kuwaingia wachezaji kwa haraka ili kusaka matokeo mazuri. Hili ni eneo la kwanza ambalo Simba limekuwa na shida.

Kuanzia Septemba 10, 2025 klabu hiyo ilipokuwa na tamasha lake la kila mwaka la Simba Day, makocha waliofundisha katika mechi rasmi za mashindano tofauti hadi sasa ni Fadlu Davids, Seleman Matola, Hemed Morocco, Dimitar Pantev na Steve Barker aliyepo hadi sasa.

Fadlu aliyeanza msimu na Simba baada ya kutua hapo tangu 2024-2025 na ndiye aliyeifikisha timu fainali ya Kombe la Shirikisho, amerejea Raja Casablanca alipotoka wakati anatua Msimbazi.

Baada ya msimu wa kwanza 2024-2025 ndani ya Simba, akaanza maisha ya 2025-2026 kwa kupoteza Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, kisha akashinda mechi ya Ligi ya Mabingwa hatua ya awali ugenini dhidi ya Gaborone United, akasepa ikiwa ni baada ya mechi mbili pekee.

Fadlu kwa kiasi kikubwa ndiye aliyefanya usajili wa kikosi cha Simba msimu huu, kufundisha mechi mbili kisha kuondoka, lilikuwa tatizo la kwanza.

Alipoondoka Fadlu, msaidizi wake, Seleman Matola akakabidhiwa kikosi kukiongoza katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara na kushinda zote dhidi ya Fountain Gate (3-0) na Namungo (3-0).

Wakati Simba ikimsaka kocha wa moja kwa moja kurithi mikoba ya Fadlu, kikosi kikaongozwa na Hemed Suleiman 'Morocco' katika mechi moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United ile ya marudiano, matokeo yakawa 1-1. Simba ikafuzu hatua ya pili.

Ndipo akatua Dimitar Pantev akianza dhidi ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini, akashinda 3-0 ugenini na nyumbani ikawa 0-0. Simba ikafuzu makundi.

Pantev aliyetambulishwa kikosini hapo Oktoba 3, 2025, akaondoka Desemba 2, 2025 baada ya kuiongoza timu hiyo katika mechi tano, kati ya hizo nne ni za Ligi ya Mabingwa Afrika na moja Ligi Kuu Bara.

Matokeo ya kupoteza mechi mbili za kundi D, yalihitimisha safari ya Pantev ndani ya Simba, timu ikawa mikononi mwa Matola tena akaiongoza kucheza dhidi ya Azam katika ligi na kupasuka 2-0.

Steve Barker akaanza maisha Simba alipotambulishwa Desemba 19, 2025, hadi sasa ameiongoza timu katika mechi tano zikiwamo tatu Kombe la Mapinduzi, moja Ligi Kuu Bara na nyingine Ligi ya Mabingwa Afrika.


Majeruhi

Eneo la pili ni ishu ya majeruhi ambapo timu hiyo imekumbwa na shida kubwa katika safu yake ya ulinzi. Kumbuka msimu uliopita wakati timu hiyo inacheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, golini kulikuwa na Moussa Camara ambaye amepata majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja muda mrefu. Pia beki wa kati Abdulrazack Hamza naye ni majeruhi.

Kuumia kwa wachezaji hao waliokuwa wakiunda ukuta wa Simba msimu uliopita, kwa kiasi fulani timu imeyumba licha ya kwamba kuna maingizo mapya yameletwa kufukia mashimo.


Wachezaji ingia, toka

Eneo la tatu katika uongozi kwani kuna uamuzi unafanyika wa haraka bila ya kutoa muda wa tathmini ya kina.

Ukiachana na kubadilisha makocha ndani ya kipindi cha muda mfupi, tatizo lingine ni namna Simba ilivyofanya usajili wa msimu uliopita na msimu huu.

Msimu uliopita, usajili ulisimamiwa na Kocha Fadlu Davids, pia msimu huu hali ikawa hiyohiyo, lakini yule aliyefanya usajili, hakudumu hali iliyoashiria wale aliowasajili wanahitaji kuingia kwenye falsafa za kocha mwingine aliyepo sasa.

Wachezaji wapya walioingia 2024-2025 chini ya Fadlu ni Joshua Mutale, Steven Mukwala, Charles Ahoua, Abdulrazack Hamza, Valentino Mashaka, Augustine Okejepha, Debora Mavambo, Omary Abdallah Omary, Valentin Nouma, Chamou Karaboue, Yusuph Kagoma, Kelvin Kijili, Awesu Awesu, Moussa Camara na Leonel Ateba. Mwisho wa msimu, Ateba, Mashaka, Okejepha, Mavambo, Omary na Kijili wameondoka.

Ukiangalia msimu huu pia, Fadlu amefanya usajili wa Rushine De Reuck, Alassane Kante, Naby Camara, Neo Maema, Morice Abraham, Yakoub Suleiman, Antony Mligo, Wilson Nangu, Jonathan Sowah, Seleman Mwalim, Mohammed Bajaber na Hussein Semfuko.

Kupitia dirisha dogo, kuna nyota walioingia mwanzoni mwa 2024-2025 wameondoka kwa sababu mbalimbali wakidumu kwa msimu mmoja na nusu ambao ni Joshua Mutale, Steven Mukwala, Charles Ahoua, Chamou Karaboue, Awesu Awesu na Moussa Camara. Pia kuna taarifa za Neo Maema na Mohamed Bajaber walioingia dirisha kubwa 2025-2026 kukatwa.

Kwa sasa dirisha dogo, tayari imetambulisha nyota wapya watano ambao ni winga Libasse Gueye, beki wa kushoto Nickson Kibabage, beki wa kati Ismaël Olivier Touré, kiungo mshambuliaji Clatous Chama na kipa Djibrilla Kassali.