Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matatu muhimu dili la Isak Liverpool

MAMBO Pict

Muktasari:

  • Isak yupo tayari kuachana na Newcastle kwenda kujiunga na Liverpool na kinachoonekana ndoto zake zinaweza kwenda kutimia.

LONDON, ENGLAND. KOCHA, Arne Slot amesema Liverpool itaendelea kufanya mchakato wa kunasa huduma ya straika wa Newcastle United, Alexander Isak katika siku za mwisho za kuelekea kufungwa kwa dirisha la usajili.

Isak yupo tayari kuachana na Newcastle kwenda kujiunga na Liverpool na kinachoonekana ndoto zake zinaweza kwenda kutimia.

Straika huyo wa Sweden aliiambia Newcastle mwishoni mwa Julai kwamba anataka kuachana na timu hiyo, lakini ofa ya awali ya Liverpool ya Pauni 110 iliyopelekwa huko St James' Park ilikataliwa.

Isak amebaki kuwa njiapanda tangu wakati huo, akigomea kuichezea timu hiyo kabla ya kuonekana akifanya mazoezi kivyake akiwa na jezi za Newcastle, lakini Liverpool bado ina matumaini kwamba itapeleka ofa ambayo itakuwa ngumu kwa miamba hiyo ya St James' Park kugomea.

Wakati sakata hilo la Isak likizidi kupambana moto, timu zinazohusika kwenye mchakamchaka huo, Liverpool na Newcastle zitakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England usiku wa Jumatatu huko St James' Park.

Liverpool tayari imeshatumia zaidi ya Pauni 300 milioni kwenye usajili wa dirisha hili la majira ya kiangazi na bado ipo kwenye mazungumzo na klabu ya Crystal Palace juu ya mpango wa kumsajili beki wa kati Marc Guehi.

Kocha Slot amewapiga bei Darwin Nunez na Luis Diaz kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huku ikimpoteza pia staa wake, Diogo Jota, aliyefariki dunia kwenye ajali ya gari, amefichua bado hajamalizana na Isak.

Alipoulizwa kama atakuwa bize kwenye siku za mwisho za kufungwa kwa dirisha la usajili, Slot alisema kwenye mkutano wa waandishi wa habari: "Sidhani, kwa sababu nitaonekana kama vile sifurahishwi na kikosi changu, mimi nafurahia kikosi changu. Nilisema wachezaji wawili kwenye kila namba, lakini wakati mwingine wanaweza kuwa wachache hivyo huwezi kuwavunja moyo wachezaji. Nafurahia kikosi changu, lakini kama kuna mchezaji ambaye tunafahamu ataweza kutufanya kuwa bora zaidi, tutamleta.

"Lakini, inapaswa kuwa vile tunavyotaka, mambo haya matatu; ada sahihi ya usajili, nafasi sahihi tunayotaka kusajili, na mchezaji atake kuja kwetu."

Liverpool kwenye vigezo hivyo vitatu, viwili vinaonekana kuwa vimekaa kwenye mstari mzuri, kwa maana ya nafasi sahihi anayotaka kusajili ni straika na mchezaji kutaka, Isak yupo tayari kujiunga kwao. Lakini, kilichobaki ni kuhusu ada sahihi ya usajili, kama itakubalika pande zote mbili, Newcastle na Liverpool ili kufanya dili hilo la Isak kutiki.

Maelezo ya Newcastle juu ya majibu yao kwa Isak ni kwamba watamuuza mchezaji huyo kama tu ada yake itakuwa sahihi, ikiaminika ada yake itaanzia Pauni 150 milioni, wakati taarifa yake ilipobainisha kwamba kila kitu kitafanyika kwa kuzingatia manufaa ya Newcastle.

Liverpool na Newcastle zitakutana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England, Jumatatu uwanjani St James' Park, mechi ambayo huenda ikawa na upinzani mkali kutokana na sakata hilo la mshambuliaji Isak.