Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manji arudi rasmi Yanga

Muktasari:

  • Tangu alipoandika barua ya kujiuzulu mwaka 2017, Yanga haikuziba nafasi yake ambapo wanachama wa klabu hiyo mara kwa mara walikuwa wakisisitiza kuwa hawajaridhia kujiuzulu kwake.

 

Baraza la wadhamini la Yanga limetangaza urejeo wa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji ambaye alijiuzulu nafasi yake mwaka jana.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo leo, mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Yanga, Kapteni George Mkuchika alisema Manji amethibitisha kuendelea kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kupitia barua aliyoandika kwenda kwa baraza hilo.

"Katika mkutano mkuu wajumbe wote 4,500 walisema wanamtaka Manji na mimi kama mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini nilimuandikia barua kumueleza kile ambacho wanachama wamekubaliana.

Sasa majibu yamekuja kwa mimi niliyemuandikia barua na katika majibu yake Manji amekubali kuendelea kuwa mwenyekiti wa Yanga," alisema Waziri Mkuchika.