Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mapya yaibuka, England yaibiwa vifaa Marekani

Muktasari:

  • Timu ya Taifa ya England itacheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Croatia, Juni 17.

Watu wawili wanashikiliwa na Polisi nchini Marekani kufuatia tukio la vifaa vya wachezaji wa timu ya Taifa ya England kuibiwa jana.

Gari lililobeba vifaa hivyo lilivunjwa na wezi hao wakati lilipokuwa njiani kuelekea Kansas City ambako ndiko kuna kambi ya timu hiyo katika kipindi chote cha Kombe la Dunia.

Vifaa vilivyoibwa katika tukio hilo ni viatu vya wachezaji, mipira, jezi na sare za mazoezi.

Inaripotiwa kwamba idadi kubwa ya jezi imeshapatikana kufuatia uchunguzi unaoendelea kufanywa na Polisi nchini humo.

Idara ya Polisi ya jiji la Kansas imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na pia kukamatwa kwa baadhi ya washukiwa.

“Watu wawili wanaohusishwa wameshawekwa ndani na uchunguzi unaendelea,” imefafanua taarifa ya idara ya Polisi.

Timu ya Taifa ya England itacheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Croatia, Juni 17.