Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki 10,000 kuiona Taifa Stars bure dhidi ya Mauritania

Muktasari:

  • Taifa Stars inaongoza msimamo wa kundi B la Fainali za CHAN 2024 ikiwa na pointi tatu.

Dar es Salaam. Ukurasa rasmi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umechapisha habari njema kwa mashabiki 10000 wa kwanza wa Mzunguko kuingia bure kutazama mchezo wa fainali za CHAN 2024 baina ya Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Mauritania katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam leo.

Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2:00 usiku huku ukitanguliwa na ule wa mapema utakaochezwa kuanzia saa 11:00 Jioni ukizihusisha timu za Taifa za Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati 

“Wanetu wa Mzunguko watu 10,000 wa kwanza mnapata ofa ya tiketi ya kuingia uwanjani bila kulipa, unachotakiwa kufanya beba Kadi yako ya N Card suala la tiketi ya kuingia tuachie sisi, utaangalia mechi zote mbili,” imefafanua taarifa ya TFF.

Aidha Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa, Neema Msitha, amesema Watanzania watakaofika leo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa watapata nafasi ya kutazama mechi mbili kwa kiingilio kimoja katika mchezo utakaochezwa saa 11:00 jioni na ule wa saa 2: 00 usiku.

Mchezo wa kwanza wa Taifa Stars ilishinda dhidi ya Burkina Faso kwa mabao 2-0.

Taifa Stars inaongoza msimamo wa kundi B ikiwa na pointi tatu ikifuatiwa na Mauritania na Madagascar zenye pointi moja kila moja huku Jamhuri ya Afrika ya Kati na Burkina Faso zikiwa hazina pointi.

Matokeo ya mchezo wa kwanza na msimamo wa kundi B ulivyo ni mambo mawili yanayoilazimisha Taifa Stars kuibuka na ushindi katika mechi hiyo ya leo ili ifikishe pointi sita ambazo zitaifanya izidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa kundi B.

Na ikiwa itafanikiwa kupata ushindi leo, Taifa Stars itahitaji ushindi angalau katika mechi moja tu au matokeo ya sare katika mechi mbili zitakazobaki dhidi ya Madagascar na Jamhuri ya Afrika ya Kati ili ijihakikishie kutinga hatua ya robo fainali.

Taifa Stars dhidi ya Mauritania 'Les Mourabitounes' ni mchezo unaokutanisha timu mbili ambazo zinafanana kwa baadhi ya mbinu kiuchezaji lakini pia zina utofauti kwa namna nyingine.

Ni timu mbili ambazo zinapendelea zaidi kutawala mchezo hasa katika safu ya kiungo lakini wakati Taifa Stars ikiwa bora zaidi katika kujilinda pindi wapinzani wanapokuwa na mpira huku Mauritania ikiwa ni timu inayopenda kushambulia kwa muda mrefu wa mchezo.