Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Simba waitika kwa Mkapa, jezi mpya kivutio

Muktasari:

  • Simba hutumia Tamasha la Simba Day kutambulisha kikosi chake cha msimu unaofuata lakini pia kufanya shughuli tofauti za kijamii.

Dar es Salaam. Idadi kubwa ya mashabiki wa Simba imejitokeza leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuadhimisha kilele cha Tamasha la Simba Day.

Katika umati huo ambao umejitokeza uwanjani hapo, asilimia kubwa ya mashabiki wamevalia jezi mpya za timu hiyo.

Kilele cha wiki ya Simba Day ni siku ambayo hutambulisha wachezaji wapya, benchi la ufundi na kuambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Ali Kiba, Yammi, Mbosso na wengine na ikihitimishwa na mechi ya kirafiki ambayo itacheza na Gor Mahia kutoka Kenya.

Imeshuhudiwa asilimia kubwa ya mashabiki waliokuja uwanjani wamevalia jezi mpya ambazo zitatumika msimu huu wa 2025/26.

Mbali na hao wapo ambao wanamiminika kwenye vibanda vya kuuzia jezi hizo wakinunua na kuvaa muda huo.

Asilimia kubwa ni jezi nyekundu zimeonekanika sehemu mbalimbali na buluu kwa baadhi ya watu huku nyeupe ikionekana sehemu chache.

Shaaban Ludewa ambaye ni muuzaji wa jezi amesema jezi hizo zinauzwa kwa bei tofauti, nyekundu na buluu ikiuzwa Sh 45,000 na nyeupe Sh 35,000.

Ludewa alisema sababu ya kuuza kwa bei tofauti ni kutokana na jezi nyekundu na buluu kuuzika zaidi kuliko nyeupe hivyo amepunguza bei ili nyeupe ipate soko.

Hata hivyo aliongeza licha ya kupunguza bei bado nyeupe iko chini kwenye mauzo, wengi wao wanainunua nyekundu na nyeupe.

"Hapa tunauza na jezi za misimu iliopita lakini hazihusiki sana wengi wananunua mpya lakini zaidi nyekundu na buluu, nyeupe wengi hawazitaki.

"Hizi nyeupe ambazo nimepunguza bei wengi wanaume, nimekuja na gari ndogo niliweka lakini nyeupe zimebaki nyingi sana,” amesema Ludewa.