Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi anarudi Ulaya kabla ya Kombe la Dunia 2026

Muktasari:

  • Manchester City imeripotiwa kuwa na nia naye mara mbili pia ukaribu wake na Pep Guardiola unaweza kufufua mazungumzo mapya.

Miami, Marekani. Supastaa wa Argentina, Lionel Messi, anatajwa kuwa katika mpango wa kutafuta mkopo wa muda mfupi Ulaya kabla ya Kombe la Dunia la 2026, kwa lengo la kupata michuano ya kiwango cha juu itakayomuweka fiti kuiongoza Argentina kutetea taji lao la Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa za ESPN Argentina, Messi ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Inter Miami nchini Marekani, anafikiria kurejea barani Ulaya kwa mkopo katika msimu wa 2025-26, ili kujinoa vyema kabla ya fainali hizo za dunia zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Ingawa mkataba wake wa sasa na Miami unamalizika mwishoni mwa mwaka huu (Desemba 2025), uongozi wa klabu hiyo inayomilikiwa na David Beckham upo katika mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya, lakini kwa sharti la kumruhusu ajiunge na klabu ya nje kwa kipindi fulani cha msimu.

Sababu ya uamuzi huo

Messi, ambaye ana umri wa miaka 38, bado ana kiu ya mafanikio makubwa akiwa na timu ya taifa ya Argentina, ambayo aliiwezesha kutwaa taji la dunia mwaka 2022 nchini Qatar. Ili awe katika ubora wa juu kimchezo, anaona ni busara kucheza soka la ushindani zaidi nje ya MLS ligi ambayo ina mapumziko marefu kuanzia Oktoba hadi Februari.

Katika chapisho lake la Instagram baada ya kufungwa na PSG 4-0 kwenye Kombe la Dunia la Klabu wiki iliyopita, Messi ameandika:

"Leo tunaaga Kombe la Dunia la Klabu baada ya kupoteza dhidi ya mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nimefurahi kuwaona tena baadhi ya marafiki wa zamani. Tunajivunia kufika hatua ya 16 bora kwenye michuano hii. Sasa ni muda wa kuelekeza nguvu zetu kwenye MLS na kila kilichoko mbele yetu."

Je, atakwenda wapi?

Kwa sasa, klabu yoyote anayoweza kujiunga nayo ni tetesi, lakini baadhi ya majina yanaibuka kama Barcelona: Ingawa Messi anahusishwa sana na klabu hiyo, uwezekano wa kurudi ni mdogo kutokana na hali ya kifedha ya klabu na mahusiano yake yaliyovunjika na Rais Joan Laporta.

Paris Saint-Germain: Tayari wamegeukia kizazi kipya kama Desire Doue hivyo kurudi kwake ni vigumu.

Manchester City imeripotiwa kuwa na nia naye mara mbili pia ukaribu wake na Pep Guardiola unaweza kufufua mazungumzo mapya.

Umuhimu wa uamuzi huu

Messi anajua anavyohitajika na Argentina, hasa baada ya kuiongoza kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2022. Kwa sasa, anataka kuhakikisha mwili wake uko kwenye kasi ya ushindani wa hali ya juu kabla ya kampeni ya mwisho ya kimataifa katika maisha yake ya soka.

Pia, kwa Inter Miami, uwepo wake umeleta mafanikio ya kibiashara na uchezaji, lakini kwa sasa maslahi ya timu ya taifa yamepewa uzito zaidi.