Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi na urithi wa milele, rekodi 12 za kihistoria Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Lionel Messi ameendelea kuimarisha nafasi yake katika historia ya Kombe la Dunia baada ya kuweka rekodi 12 zinazomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji walioacha alama kubwa zaidi katika mashindano hayo.

Lionel Messi si jina geni katika historia ya soka duniani, lakini kila anapoweka rekodi mpya huendelea kuthibitisha kwa nini ametajwa miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kutokea.

Katika jukwaa kubwa zaidi la soka duniani, Kombe la Dunia, nahodha huyo wa Argentina ameacha alama ya kipekee kwa kuweka rekodi ambazo huenda zikachukua muda mrefu kuvunjwa. Kutoka kwenye mabao, pasi za mwisho hadi mafanikio binafsi, safari ya Messi katika Kombe la Dunia imekuwa simulizi ya kipaji, uvumilivu na urithi wa kizazi.

Messi anashikilia rekodi ya kutoa pasi nyingi zaidi za mabao katika historia ya Kombe la Dunia akiwa na 12, huku pia akiwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi katika mashindano hayo akiwa amefunga jumla ya mabao 21.

Mbali na hilo, nyota huyo anaongoza kwa mchango mkubwa zaidi wa mabao katika historia ya Kombe la Dunia, akiwa amehusika moja kwa moja kwenye mabao 33 kupitia kufunga na kutoa pasi za mwisho.

Mafanikio mengine makubwa ya Messi ni kuwa mchezaji pekee aliyewahi kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia mara mbili, jambo linaloonyesha kiwango chake cha juu katika vipindi tofauti vya maisha yake ya soka.

Katika rekodi za ufanisi wa kufunga, Messi ndiye mchezaji aliyefunga katika mechi nyingi zaidi za Kombe la Dunia akiwa na mechi 16, huku pia akiweka rekodi ya kufunga katika mechi tisa mfululizo za mashindano hayo.

Aidha, mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2022 amefunga dhidi ya mataifa 15 tofauti katika michuano hiyo, idadi ambayo haijafikiwa na mchezaji mwingine yeyote.

Katika hatua za mtoano, Messi anaendelea kutawala takwimu baada ya kuwa na rekodi ya pasi nyingi za mabao 10, huku akiwa na mchango wa mabao 17 katika hatua hiyo.

Mbali na hayo, Messi ameweka historia kwa kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga mabao matatu katika mechi moja (hat-trick) katika Kombe la Dunia akiwa na miaka 38, huku pia akiwa miongoni mwa wachezaji wenye mabao mengi ya mipira ya adhabu ya moja kwa moja katika historia ya mashindano hayo akiwa na mawili.

Rekodi nyingine ya kipekee ni kuwa Messi ndiye mchezaji pekee aliyefunga katika kila hatua ya toleo moja la Kombe la Dunia, jambo lililoonyesha mchango wake mkubwa katika safari ya Argentina kutwaa ubingwa mwaka 2022.

Kwa rekodi hizo, Messi ameendelea kuandika ukurasa mpya katika historia ya Kombe la Dunia kama mmoja wa wachezaji wakubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka.

Ikumbukwe staa huyo katika fainali za Kombe la Dunia 2026 anaongoza chati ya ufungaji bora akiwa na mabao nane sawa na Kylian Mbappe huku akiisaidia Argentina kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo.

Argentina itavaana na Hispania Jumapili Julai 19, 2026 katika Uwanja wa MetLife ikiingia kutetea ubingwa wake wa Kombe la Dunia.