Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshahara wa Messi pasua kichwa

Nyota wa Inter Miami, Lionel Messi. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Vilevile katika mkataba wake ana kipengele kinachompa haki ya kumiliki sehemu ya hisa ya klabu hiyo katika siku zijazo.

Florida, Marekani. Mabosi wa Inter Miami wanapambana kutafuta wadhamini watakaowekeza katika timu yao kutokana na gharama kubwa za uendeshaji wa klabu zinazowakabili ikiwamo mshahara wa Lionel Messi.

Mapema wiki iliyopita, mmiliki mwenza wa Inter Miami, Jorge Mas alikiri nyota huyo wa kimataifa wa Argentina analipwa takribani Dola 70 milioni kwa mwaka kijumla.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka The Athletic, Mas amesema kwa sasa wanatafuta wadhamini zaidi kwa sababu gharama zimekuwa kubwa.

"Sababu inayofanya nihitaji wadhamini wakubwa wa kiwango cha dunia ni wachezaji tulionao ni ghali. Namlipa Messi kati ya Dola 70 hadi 80 milioni kwa mwaka."

Kwa mujibu wa MLS Players Association, mshahara pekee wa Messi ni Dola 12 milioni kwa mwaka, lakini unazidi zaidi kutokana na mjumuisho wa bonasi na gharama nyingine za kumhudumia.

Vilevile katika mkataba wake ana kipengele kinachompa haki ya kumiliki sehemu ya hisa ya klabu hiyo katika siku zijazo.

Gwiji huyo wa Argentina alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu Oktoba mwaka jana unaomhakikishia kuendelea kusalia katika klabu hiyo ya Florida hadi mwaka 2028.

Tangu alipowasili Marekani, Messi amekuwa na wakati mzuri katika kikosi cha Inter Miami akiiongoza kutwaa ubingwa wa MLS mwaka 2025, akifunga mabao 29 na kushinda tuzo ya mfungaji bora (Golden Boot) katika msimu huo uliokuwa wa kipekee.

Messi pia anaongoza kama mchezaji anayelipwa zaidi katika MLS.

Hata hivyo, mapato hayo makubwa bado hayafikii kiwango cha fedha anacholipwa mpinzani wake wa karibu, Cristiano Ronaldo wa Al Nassr ya Saudi Arabia.

Nyota huyo wa Ureno alisaini mkataba mpya wa miaka miwili na Al-Nassr FC Juni mwaka jana, utakaomuweka jijini Riyadh hadi mwaka 2027.

Ilifichuliwa mkataba huo utamwezesha kupata takribani  Pauni 178 milioni kwa mwaka ambayo ni karibu mara tatu ya mapato ya Messi kwa mwaka.

Dili hilo la Ronaldo linatajwa kuwa miongoni mwa mikataba yenye thamani kubwa zaidi katika historia ya soka, huku akiripotiwa kulipwa takribani Pauni 488,000 kwa siku.

Kwa ujumla, Ronaldo analipwa takriban Pauni 492 milioni katika kipindi cha miaka miwili kwa mshahara, bonasi na marupurupu mengine.