Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Paredi la Yanga...Jiji linasimama

Muktasari:

  • Huu ni ubingwa wa 31 inautwaa Yanga ambayo ndiyo timu iliyotwaa ubingwa huo mara nyingi zaidi ikifuatiwa na Simba iliyouchukua mara 22.

Yanga leo inatarajiwa kuliteka jiji la Dar es Salaam wakati itakapokuwa ikifanya paredi baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/2024, Kombe la FA, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano pamoja na Kombe la Toyota.

Yanga ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa bara baada ya kukusanya pointi 82 zikiwa ni nne mbele ya mtani wao wa jadi Simba ambao walikusanya pointi 78, na kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Huu umekuwa ubingwa wa nne mfululizo kwa Yanga na paredi ililifanya baada ya kutwaa ubingwa msimu uliopita lilivunja rekodi ya mahudhuria makubwa ya mashabiki huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kile ambacho kitafanyika leo.

Jana timu hiyo ilivaana na Singida Black Star kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho la CRDB uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar na kupata ushindi wa mabao 2-0 na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa sherehe hizo zitaanza baada ya kikosi cha timu hiyo kutua Uwanja wa Ndege Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya paredi hilo, Mkuu wa Kitego cha Habari wa Yanga, Ally Kamwe, amesema msimu huu kutakuwa na utaratibu wa tofauti na mingine iliyopita kwa kuwa wameongeza vituo vingine vya kusimama na mashabiki wote wa timu hiyo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi.

Akitaja utaratibu wa paredi hilo, Kamwe alisema wachezaji wao mastaa Clatous Chama, Jonas Mkude na Israel Mwenda watasimama juu ya gari watakapofika mitaa ya Msimbazi ili wahutubie taifa.

"Msimu huu tumepitia mengi sana kama klabu. Lakini siri yetu ya mafanikio, licha ya mawimbi makubwa ni umoja na mshikamano umetusaidia. viongozi ambao tuliwaamini watusaidie kwenye nyakati ngumu wamefanikisha hilo na tumevuka salama.

"Siamini kama kuna Mwanayanga atabaki nyumbani Jumatatu asije kusherehekea mafanikio ya klabu yake, kwa tuliyoyapita.

"Paredi za miaka iliyopita tulikuwa tunasimama kituo kimoja tu, lakini msimu huu tutakuwa na vituo vitatu, awali Msimbazi tulikuwa tunasimama dakika tano tu lakini msimu huu tutakaa hapo masaa matatu ili mastaa wetu, Clatous Chama, Israel Mwenda na wakati mwingine Mkude wasimame kwenye gari ili kuhutubia taifa," alisema Kamwe.

Yanga imetwaa ubingwa huo ikiwa imepoteza michezo miwili tu msimu mzima ilipochapwa na Tabora United na Azam FC, ilifanikiwa kufungwa mabao 10 na yeyewe kufunga 83, ikitoka sare michezo miwili.

Huu ni ubingwa wa 31 inautwaa Yanga ambayo ndiyo timu iliyotwaa ubingwa huo mara nyingi zaidi ikifuatiwa na Simba iliyouchukua mara 22.