Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Barcelona amwangukia Xavi

Muktasari:

  • Xavi, 44, alithibitisha kwamba anaondoka mwezi uliopita ambapo alisema amefanya uamuzi huo muda mrefu na kusisitiza ataondoka hata kama timu hiyo ikishinda Ligi ya Mabingwa.

Barcelona, Hispania. Rais wa Barcelona amemuomba kocha wa timu hiyo Xavi kuendelea kusalia kama kocha mkuu licha ya kutangaza kwamba ataondoka mwisho wa msimu.

Xavi, 44, alithibitisha kwamba anaondoka mwezi uliopita ambapo alisema amefanya uamuzi huo muda mrefu na kusisitiza ataondoka hata kama timu hiyo ikishinda Ligi ya Mabingwa.

"Hali unayojisikia ukiwa kocha wa Barcelona huwa  mbaya sana, unakutana na vitendo vingi vya kukuvunjia heshima jambo ambalo linakuathiri kisaikolojia, unavumilia na mwisho unakuja kuangukia kwenye uamuzi kama huu."

Xavi alitangaza hivyo baada ya kuibuka kwa tetesi  kwamba mkurugenzi wa ufundi wa Barcelona  Deco anataka kumfukuza na kumpandisha Rafa Marquez ambaye anafundisha timu za vijana za Barca kwa sasa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Barcelona ni kwamba rais wa timu hiyo Joan Laporta hajakata tamaa juu ya Xavi na matumaini ya kwamba atamshawishi abaki kwenye timu hiyo.

Inaelezwa kwamba makamu wa rais wa Barca Rafa Yuste, amejaribu kumshawishi Xavi aendelee kuifundisha timu hiyo hadi pale mkataba wake utakapomalizika mwaka 2025.

Vigogo wanajaribu kumshawishi Xavi akubali kubakia kwa sababu wanakumbana na wakati mgumu kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya.

Inadaiwa makocha wengi wamekuwa wakikataa ofa ya Barca kwa sababu ya ukata wao wa kifedha unaowakumba kwa sasa.
Vilevile mabosi wa timu hiyo wamekuwa wakihitaji makocha wahakikishe timu inashinda mataji bila ya kuzingatia suala hilo la ufinyu wa maboresho ya kikosi.

Hata hivyo Xavi, ambaye aliiwezesha Barca kushinda taji la La Liga amekanusha taarifa za kwamba ataendelea kuifundisha timu hiyo.

"Nafikiri timu imezidi kwenda mbele tangu nitangaze kwamba naondoka, wachezaji wamekuwa wakijituma sana na mashabiki wanaimba jina langu lakini bado naamini kwamba uamuzi wangu ni sahihi, nashukuru kwamba mashabiki wamekuwa upande wangu"