Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford acheza mechi ya kwanza Barcelona

Muktasari:

  • Kama mambo yataenda sawa, huenda mshambuliaji huyo akapewa mkataba wa kudumu Nou Camp mwishoni mwa msimu.

Barcelona, Hispania. Nyota wa zamani wa Manchester United, Marcus Rashford, ameanza maisha mapya nchini Hispania baada ya kuichezea Barcelona kwa mara ya kwanza katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Vissel Kobe ya Japan, katika mechi ya kirafiki.

Rashford (27), aliingia uwanjani kipindi cha pili akiwa amevalia jezi namba 14, namba ambayo iliwahi kuvaliwa na gwiji wa klabu hiyo, Thierry Henry. Hata hivyo, hakuweza kukamilisha dakika 45, kwani alitolewa dakika ya 78.

Nyota huyo wa kimataifa wa England alikuwa sehemu ya kikosi kilichotengwa Manchester United msimu huu wa maandalizi, kabla ya kujiunga rasmi na miamba hiyo ya Catalonia kwa mkopo wa msimu mmoja, huku kukiwa na kipengele cha kununuliwa moja kwa moja mwishoni mwa msimu.

Rashford ambaye alitambulishwa kupitia video inayomuonesha ndani ya kibanda maarufu cha simu cha England, alisema:

 “Nina furaha kubwa. Hii ni klabu ambayo ndoto za watu hutimia. Imani na misingi ya klabu hii vinaendana na maisha yangu. Najisikia kama niko nyumbani. Ni klabu ya kifamilia na ni mazingira rafiki kwa mchezaji kuonesha kipaji chake.”


Aliongeza kuwa:

“Nilikuwa shabiki wa Barcelona tangu utotoni. Ni klabu inayopenda soka safi. Nitafurahia kila dakika nitakayovaa jezi hii.”

Rashford anatarajia kushiriki mechi mbili zaidi za maandalizi nchini Korea Kusini kabla ya kurejea Hispania kwa mchezo dhidi ya Como. Barcelona itaanza rasmi kampeni ya kutetea ubingwa wa La Liga Agosti 16 dhidi ya Mallorca.

Kama mambo yataenda sawa, huenda mshambuliaji huyo akapewa mkataba wa kudumu Nou Camp mwishoni mwa msimu.