Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Refa Yanga, Belouizdad shughuli pevu

Muktasari:

  • Traore ndiye amepangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kushika kipyenga katika mechi hiyo akisaidiwa na Sydou Tiama (Burkina Fasso), Nodibo Samake (Mali) na refa wa mezani Ousmane Diakate kutoka Mali.

Historia ya refa Boubou Traore (34) kutoka Mali, inazilazimisha Yanga na Belouizdad kila moja kujipanga vilivyo wakati zitakapokutana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Jumamosi kuanzia saa 1:00 usiku.

Traore ndiye amepangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kushika kipyenga katika mechi hiyo akisaidiwa na Sydou Tiama (Burkina Fasso), Nodibo Samake (Mali) na refa wa mezani Ousmane Diakate kutoka Mali.

Refa huyo ameonekana kuwa na historia ya bahati kwa timu za kutoka ukanda wa nchi zinazozungumza lugha ya Kiarabu lakini pia amekuwa na kumbukumbu mbaya kwa CR Belouizdad katika mechi ambazo huwa wanachezeshwa naye.

Katika mechi 10 zilizopita ambazo timu za Kiarabu zilicheza huku refa akiwa Traore, ziliibuka na ushindi mara tisa na moja ikitoka sare.

Lakini pamoja na timu nyingi kutoka Uarabuni kuwa na historia ya kufanya vyema pindi zinapochezeshwa na Traore, refa huyo amekuwa na nuksi kwa Belouizdad kwani haijawahi kupata ushindi au hata sare pale alipowachezesha.

Traore amechezesha mechi mbili za Belouizdad ambazo ya kwanza ni ile waliyocheza Februari 28, 2021 na Mamelodi Sundowns kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa ambayo timu hiyo kutoka Algeria ilichapwa mabao 5-1.

Februari 24, 2023, CR Belouizdad ilipoteza kwa bao 1-0 mbele ya Al Merrikh huku refa wa mchezo akiwa ni Boubou Traore.

Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika, inahitaji ushindi katika mechi hiyo dhidi ya Belouizdad ili ifikishe pointi nane na kuweka hai matumaini yake ya kuingia hatua ya robo fainali.

Kwa sasa, msimamo wa kundi hilo unaongozwa na Al Ahly ya Misri yenye pointi sita, ikifuatiwa na Belouizdad kisha Yanga ambazo zina pointitano kila moja na Medeama iko mkiani na pointi zake nne.