Samatta arudisha majeshi Genk

BAADA ya miaka miwili, miezi saba na siku 16 hatimaye Mbwana Samatta amerejea tena KRC Genk, timu ya kwanza kuichezea barani Ulaya na kupata mafanikio makubwa ikiwa pamoja na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu nchini Ubelgiji.
Samatta amereja Genk kwa mkopo wa msimu mmoja wenye kipengele cha kumnunua mazima akitokea Fenerbahce ambako hakuwa anapata nafasi ya kucheza tangu alipotua akitokea Aston Villa.
Hii itakuwa ni mara yapili Samatta kutolewa kwa mkopo na Fenerbahce baada ya mara ya kwanza kupelekwa Royal Antwerp ya huko nchini Ubelgiji.
Mkataba wa sasa wa staa huyu na Fenerbahce  unatarajiwa kumalizika mwaka 2024.
Mbali ya kuchukua ubingwa akiwa na Genk msimu wa 2018/19, Samatta pia aliibuka kuwa mfungaji bora baada ya kuingia kambani mara 20.