Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sare ilivyosogeza mbele ubingwa wa Ronaldo Saudi Arabia

Nyota wa Al-Nassr , Cristiano Ronaldo wakati akionekana mwenye masikitiko baada ya timu yake kushindwa kuondoka na ushindi katika mechi ya Ligi Kuu Saudi Arabia dhidi ya Al Hilal. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Ronaldo atasubiri hadi mechi ya mwisho ambapo Al Nassr itahitaji ushindi dhidi ya Damac FC ili kutwaa taji la Ligi Kuu Saudi Arabia.

Riyadh, Saudi Arabia. Nyota wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, alionekana mwenye majonzi makubwa baada ya ndoto ya Al-Nassr kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Saudi Arabia ‘Saudi Pro League’ kucheleweshwa katika dakika za za majeruhi kufuatia bao la kujifunga lililowapa uhai wapinzani wao Al Hilal.

Al-Nassr ilikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Mohamed Simakan, matokeo ambayo yalionekana kuiweka timu hiyo karibu kutwaa ubingwa baada ya miaka saba.

Ronaldo mwenye miaka 41 alitolewa dakika saba kabla ya mchezo kumalizika huku mashabiki wakimshangilia katika Uwanja wa Al-Awwal Park.

Hata hivyo, katika dakika ya nane ya nyongeza, kipa Bento Matheus Krepski alitoka kuokoa mpira wa kurusha, lakini alifanya makosa baada ya kugongana na beki Íñigo Martínez, na mpira ukaingia wavuni kwa bao la kujifunga lililoisawazishia Al-Hilal.

Baada ya mchezo huo, kamera zilimuonyesha Ronaldo akiwa amekaa peke yake kwenye benchi la Al-Nassr akiwa mwenye huzuni kubwa huku mchumba wake, Georgina Rodríguez, pamoja na watoto wake wakishuhudia tukio hilo kutoka jukwaani.

Georgina Rodriguez ambaye ni chumba wa nyota wa Al Nassr, Cristiano Ronaldo alipokuwa kwenye jukwaa pamoja na watoto wao wakifuatilia mechi ya Ligi Kuu Saudi Arabia kati ya Al Nassr na Al Hilal. Picha na Mtandao

Ronaldo ambaye ameifungia Al-Nassr mabao 127 katika mechi 146 tangu ajiunge nayo mwaka 2022, bado anasubiri kutwaa ubingwa wake wa kwanza mkubwa Saudi Arabia.

Hadi sasa, taji pekee aliloshinda akiwa nchini humo ni Arab Club Champions Cup mwaka 2023.

Licha ya sare hiyo, Al-Nassr bado inaongoza mbio za ubingwa ikiwa na tofauti ya pointi tano dhidi ya Al-Hilal, huku ikiwa imesalia na mchezo mmoja dhidi ya Damac FC utakaofanyika wiki ijayo Mei 21, 2026. Ushindi katika mchezo huo utaipa Al-Nassr ubingwa wa kwanza wa ligi tangu mwaka 2019.