Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sare yamchefua beki Man United

Manchester, England. Manchester United imeduwazwa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na timu inayoburuza mkia ya Wolves, jambo lililomchefua beki wa timu hiyo, Lisadro Martinez alionekana kuwa na hasira kutokana na uzembe uliofanywa na kusababisha kushindwa kupata ushindi mbele ya vibonde haop wa Ligi Kuu ya England.

Wolves iliambulia pointi yake ya tatu msimu huu katika mechi 19 za EPL baada ya sare hiyo ya Old Trafford na hivyo kuigomea Man United nafasi ya kutinga Top Four.

Man United sasa imeangusha pointi tisa kutoka katika mechi tano za mwisho ilizocheza Old Trafford ndani ya wiki sita. Na mechi hiyo ya Wolves ilikuwa mara ya sita kwa Man United kuongoza 1-0 msimu huu na kisha kushindwa kutoka na pointi zote tatu za ushindi.

Martinez, ambaye alikuwa nahodha wa Man United katika mechi ya pili mfululizo kutokana na Bruno Fernandes kuwa majeruhi alisema: “Nimehuzunika sana. Hatuwezi kuja hapa na kutoka sare nyumbani katika mechi kama hii. Yatupasa kushinda nyumbani. Wapinzani lazima wataabike, lakini hatukupata pointi tatu. Inakera sana."

Beki huyo aliongeza kwa kusema; “Timu ilijitolea kila kitu. Muda mfupi tu, tuliruhusu bao dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, hilo linatokea. Tulistahili, yatupasa kuwajibika. Wolves hawastahili ile nafasi wanayoshika, wana timu imara. Tuliwaheshimu. Sote tumehuzunika, tulitarajia matokeo mazuri. Lazima tukubaliane na hilo na kujiandaa na mchezo mwingine.”

Man United ilikosa huduma ya wachezaji wanane wa kikosi cha kwanza, lakini kocha Ruben Amorim hataki kulichukua hilo kama kisingizio kwa sababu iliichapa Newcastle United katika Boxing Day ikiwa haina wachezaji saba.

Amorim mwenye umri wa miaka 40, alisema: “Hatukutumia hiki kisingizio dhidi ya Newcastle. Hatuwezi kukitumia pia kwenye mechi hii, ukiangalia mchezo utaona kwanini tumecheza tulivyocheza, hatukuwa kwenye ubora wetu na tulipoteza mara nyingi kwenye matukio ya ana kwa ana.”

Baada ya kuachana na fomesheni ya 3-4-2-1 katika mechi ya Newcastle na kucheza 4-2-3-1, Amorim alirudi tena na mtindo wa mabeki watatu dhidi ya Wolves na alipoulizwa kuhusu kurudi tena katika 3-4-2-1 alisema: “Tulijua watacheza na watu watano kati. Watatumia mawinga na wamefanya hivyo.”