Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys yatawala kikosi bora AFCON

Muktasari:

  • Serengeti Boys ilipoteza mechi ya Fainali ya AFCON U17 2026 kwa kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Senegal baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Licha ya kukosa ubingwa wa Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) 2026, Serengeti Boys imetamba kwa kuingiza idadi kubwa ya wachezaji katika kikosi bora cha mashindano hayo.

Jopo la tathmini ya ufundi ya mashindano hayo, limeteua wachezaji wanne wa Serengeti Boys katika kikosi bora cha mashindano hayo yaliyomalizika kwa Senegal kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3.

Mabingwa wa mashindano hayo, Senegal nao wametoa idadi sawa na ile ya Serengeti Boys, Morocco ikitoa wawili na mwingine akitokea Misri.

Kama iliyotegemewa, Mchezaji Bora wa mashindano hayo, Issa Chole, yumo katika kundi hilo la wachezaji wanne wa Serengeti Boys ambao wamepata fursa hiyo ya heshima ya kutambuliwa kama nyota 11 bora wa mashindano.

Nyota mwingine wa Serengeti Boys ambaye ameingia katika kikosi cha wachezaji bora wa AFCON U17 ni Mfungaji Bora wa mashindano hayo, Athanas Adam huku pia akiwepo winga Razack Mbegelendi na beki Hussein Mbegu.

Kipa Bora wa mashindano hayo, Assane Sarr anaongoza kundi la wachezaji wanne wa Senegal ambao wameteuliwa kuwemo katika kikosi hicho.

Nyota wengine wa Senegal waliomo katika kikosi hicho ni beki wa kushoto, Lamine Mbengue na beki wa kulia, Thierno Sow pamoja na winga Mouhamed Wagne.

Beki wa kati, Adam Soudi na mshambuliaji Mohamed Moustache wa Morocco nao wapo kikosini.

Misri ina mchezaji mmoja kwenye kikosi hicho bora cha mashindano ambaye ni kiungo Abdelrahim Omar.

Wachezaji 11 wanaounda kikosi hicho ni Assane Sarr, Thierno Sow, Lamine Mbengue, Adam Soudi, Hussein Mbegu, Issa Chole, Razack Mbegelendi, Abdelrahim Omar, Mohamed Moustache, Athanas Adam, Mouhamed Wagne