Twiga yaishangaza Zimbabwe Cosafa
Muktasari:
- WAKATI wadau wengi wa soka la Wanawake wakiamini kwamba timu ya Taifa ya Tanzania kwa upande wa Wanawake 'Twiga Stars' ingepata ugumu kwenye mchezo wake wa kwanza wa kundi B dhidi ya Zimbabwe mambo yamekuwa tofauti.
WAKATI wadau wengi wa soka la Wanawake wakiamini kwamba timu ya Taifa ya Tanzania kwa upande wa Wanawake 'Twiga Stars' ingepata ugumu kwenye mchezo wake wa kwanza wa kundi B dhidi ya Zimbabwe mambo yamekuwa tofauti.
Tanzania ilifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Cosafa inayofanyika huko Afrika ya Kusini.
Katika mchezo huo bao la kwanza la Tanzania lilifungwa na Donisia Minja dakika ya 42 baada ya kuunganisha mpira
uliokolewa na kipa wa Zimbabwe.
Baada ya bao hilo Tanzani iliendelea iliendelea kulisakama lango la Zimbabwe lakini hakuna bao lililoingia hadi kipindi
cha kwanza kinamalizika.
Katika kipindi cha pili Twiga ilianza kwa moto ule ule iliomaliza nao katika kipindi cha kwanza na ilikuwa dakika ya 51
Dian Lucas alipiga pasi safi kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mwanahamisi Omary aliyekokota mpira kwa mita kadhaa kisha akapiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango na kuiandikia Tanzania bao la pili.
Zimbabwe ilifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwaingiza Natasha Ndowa na Maudy Mafuruse lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote kwenye uchezaji wao na Tanzania ilizidi kulisakama lango lao.
Dakika ya 65, kocha wa Twiga Bakari Shime alifanya mabadiliko kwa kumtoa Opa Clement na kumuingiza Aisha Masaka.
Wakati mchezo unaonekana kuwa unakwenda mwishoni Aisha Masaka alipokea pasi kutoka kwa Mwanahamisi na kumaliza kabisa mchezo kwa kufunga bao la tatu.
Mwanahamisi aliibuka mchezaji bora wa mchezo na katika mahojiano aliyofanya baada ya mechi alisema; "Ushindi huu
unatokana na kazi kubwa tuliyofanya kama timu na kuifunga Zimbabwe kwetu sio kama tunajua sana bali imetokana
na umoja wetu, najisikia furaha sana kuchukua tuzo hii na kwangu imenishangaza kwani sikutarajia"
Kocha wa Zimbabwe Sithethelelwe Sibanda naye baada ya mchezo alisema; "Tumecheza vizuri lakini tulifanya baadhi
ya makosa ambayo ndio yamesababisha tupoteze mechi kwa sababu tuliadhibiwa, kwangu eneo la ushambuliaji ndio
lilikuwa linashida lakini tumeona mapungufu na tutafanyia kazi, hivyo tunarajia kufanya vizuri kwenye mchezo ujao."
Vilevile kocha wa Tanzania Bakari Shime alisema; "Ulikuwa mchezo mgumu kwetu hasa katika kipindi cha kwanza kwa
sababu uwanja ulikuwa umeloa sana hivyo ikawa ngumu kucheza mpira tulivyozoea, lakini katika kipindi chapili tulirudi
kwenye mchezo wetu na kupata matokeo tuliyoyapata. Matokeo haya yametujengea hali ya kujiamini kuelekea mchezo
ujao."
Ushindi huo umeifanya Tanzania kushika nafasi ya pili kwenye kundi B, nyuma ya Botswana kwa tofauti ya mabao,
kwa sababu Botswana iliifunga Sudani ya Kusini mabao 7-0.
Mchezo ujao Twiga itakutana na Botswana Oktoba mbili saa 7:00.