Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Udogo wa Curacao na rekodi mpya Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Curacao ikiwa ni taifa dogo zaidi kuwahi kufuzu Kombe la Dunia imeendea kuandika rekodi mpya katika mashindano ya 2026 ikipata pointi.

Curacao imefanikiwa kupata pointi ya kwanza ya kihistoria kwenye Kombe la Dunia baada ya kulazimisha sare  ya bila kufungana dhidi ya Ecuador.

Ecuador itajilaumu yenyewe kushindwa kutengeneza ushindi kwenye mchezo huo kutokana na kuwa na nafasi nyingi za kufunga, lakini ikashindwa kuzitumia.

Kipa wa Curacao, Eloy Room ndiye mchezaji ambaye  atakuwa amewaumiza Ecuador akiwa shujaa wa taifa lake baada kufanya kazi bora ya kuzuia timu yake kuruhusu bao.

Room mwenye umri wa miaka 37 alifanya kazi nzuri ya kupangua mashambulizi 15 akiwapa wakati mgumu mastaa wa Ecuador katika mashambulizi yao.

Ecuador imetawala vyema mchezo huo ikionyesha umiliki mzuri wa mchezo kwa vipindi vyote viwili.

Mshambuliaji Enner Valencia atajilaumu kwa kupoteza nafasi tatu za wazi za kufunga akiwa uso kwa uso na kipa huyo.

Matokeo hayo yanaibakiza Curacao chini ya msimamo wa kundi E ikiwa nafasi ya nne juu wakiwepo Ecuador ambao nao wana pointi moja, Ivory Coast ikishika nafasi ya pili na pointi tatu huku vinara wakiwa Ujerumani wenye pointi sita. Timu zote zimecheza mechi mbili.