Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Al Ahly zatumiana salamu kwa dozi sawa

Muktasari:

  • Yanga itaikaribisha Al Ahly katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Jumamosi, Januari, 31, 2026 katika mechi ya raundi ya nne ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga na Al Ahly zimepata ushindi unaofanana katika mechi za Ligi kwenye nchi zao hapo jana Jumanne, Januari 27, 2026 huku zikiwa zimebaki siku nne kabla ya kukutana kwenye mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 sawa na ule ambao Al Ahly imeupata katika Ligi Kuu ya Misri.

Katika Uwanja wa KMC, Yanga imeichapa Dodoma Jiji FC kwa mabao 3-1 ambao umeifanya ifikishe pointi 22 na kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi.

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Laurindo Aurélio maarufu Depu akijaribu kuwatoka mabeki wa Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa jana Jumanne Januari, 27, 2026 katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam. Picha na Yanga

Nyota wa mchezo kwa Yanga alikuwa ni Depu ambaye ameifungia mabao mawili huku bao lingine moja likipachikwa na Prince Dube.

Mabao hayo mawili yanamfanya Depu afikishe idadi ya mabao matatu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ameicheza kwa mechi mbili tu tangu alipojiunga na Yanga.

Bao moja la Dodoma Jiji katika mechi hiyo limepachikwa na mshambuliaji William Edgar.

Mshambuliaji wa Al Ahly, Zizo na Mahmoud Trézéguet wakishangilia moja ya bao katika ushindi wa 3-1 mechi ya Ligi Kuu Misri dhidi ya Wadi Degla jana Jumanne, Januari 27, 2026. Picha na Mtandao

Nchini Misri, Al Ahly imeutumia vyema Uwanja wake wa nyumbani wa Al Salam jijini Cairo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Wadi Degla.

Walioifungia mabao Al Ahly jana ni Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’, Zizo na Marwan Otaka huku bao pekee la Wadi Degla likipachikwa na Ahmed Mostafa Sayed.

Ushindi huo umeifanya Al Ahly ifikishe pointi 26 na kusogea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Misri.