Watumishi tisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, akiwamo aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Amos Kusaja na wafanyabiashara watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh205.7 milioni.