Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Padri Dk Charles Kitima amewaita mbele ya kongamano la tano la Ekaristi Takatifu, Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi na Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara, Tundu Lissu pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kwa ajili ya kusalimia waumini.