Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba ametembelea ofisi za Mwananchi Communications Limited (MCL) zilizopo Relini Jijini Dar es Salaam, leo Agosti 16, 2024.
Makoba amepokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Bakari Machumu ambapo wamezungumzia mambo mbalimbali ya kushirikiana na namna bora ya kujenga Taifa.