Mazishi ya Thadei Ole Mushi yamefanyika leo Februari 07, 2024, nyumbani kwake katika Kijiji cha Shinga, Uru Kusini, wilayani Moshi. Maziko hayo ya mchambuzi na aliyeiteka mitandao ya kijamii kwa mada mbalimbali, Thadei yamewakutanisha viongozi wa kisiasa kutoka vyama mbalimbali mkoani Kilimanjaro, huku wakimtaja kama kijana shupavu aliyesimamia ukweli bila woga. Picha na Ombeni Daniel