Rais Samia Suluhu Hassan akimfariji muathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh, Salome Elifuraha ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini iliyopo Katesh, Hanang.
Mama huyo amepoteza watoto wake wawili kwenye maporomoko ya tope yaliyotokea Mlima Hanang Jumapili Desemba 3, 2023.