Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan amezidua Ilani mpya ya uchaguzi ya CCM kwa mwaka 2025 - 2030 baada ya wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa chama hicho kuipitisha jijini Dodoma leo Mei 30, 2025. Baada ya tukio hilo Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Stephen Wasira amekabidhi Ilani hiyo kwa mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia, mgombea mwenza, Dk Emmanuel Nchimbi na mgombea urais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi. Picha na Edwin Mjwahuzi