Waombolezaji waliojitokeza katika Viwanja vya Leaders Club wamekumbwa na hali ya simanzi na vilio wakati wa kuaga mwili wa mwigizaji Grace Mapunda maarufu ‘Tesa wa Huba’, leo Novemba 4, 2024. Grace alimefariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 2, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika chumba cha wagonjwa mahututi, kwenye Hospitali ya Mwananyamala. Picha zote na Michael Matemanga