Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango leo Agosti 26, 2024 amefungua wiki ya nenda kwa usalama barabarani na maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Mpango amesema ukaguzi wa magari unapaswa kuwa endelevu na kufanyika kwa mwaka mzima badala ya kusubiri hadi kwenye Wiki ya Usalama barabarani Kitaifa. Picha na OMR